Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 390
- 1,425
Nimehuzunishwa sana na kitendo cha shabiki wa Yanga kumtandika ngumi ya uso mwanachama wa Simba Doctor Mohamed akiwa anahojiwa na chombo cha habari, shabiki huyo aliyekuwa amefuatana na Ally Kamwe wakiwa wanatoka uwanjani alimtandika kibao dokta Mohammed kufuatia Yanga kuondolewa mashindanoni.
Ally Kamwe aliangalia tukio hilo na akarudi nyuma kumuomba radhi Doctor Mohamed kwa kitendo hicho.
Nimefurahi sana kwa kitendo hicho cha Ally Kamwe. Ndugu zangu mashabiki, Yanga kutolewa leo imekuwa nongwa hadi mnapiga mashabiki kweli?
Hasira za nini, kwa mfano wewe uliyempiga kibao Doctor Mohamed unajulikana maana social media zote zimekumulika, akienda kuripoti polisi kuwa umemshambulia, amepoteza simu Iphone 16, umemvunja taya, huoni atavunja kibubu chako, hongera Kamwe umekuwa muungwana mnooooo.