Nawashukuru sana kwa kuliona tatizo la Rage, lakini ni sahihi kumlaumu yeye binafsi?
Mie nipo tofauti kidogo na naona wa kulaumu ni wale wanaompa kila akitakacho:-
1. Wakazi wa Tabora= pale ana vyeo vingi mno kana kwamba hawaoni hakuna mwingine ila yeye kama ni muarobaini.
2. Wanachama wa Simba= katiba ya klabu ilikiukwa kwani rage ni mkaaji wa Tabora, sasa ni mbunge.
3. TFF= kumruhusu kuingia uwanja wetu wa taifa na jamaa zake wa klabu ndogo ya England eti kuukagua. Haya ni matusi kwetu watanzania, uwanja huu si wa klabu yoyote ni wa wananchi mbona FIFA/CAF na hata CECAFA wameuidhinisha kwa mashindano yao mengi tu kufanyika hapo hata timu bora kabisa kwa soka ya taifa linaloheshimika la Brasil imecheza hapo sasa haiingii akilini leo watu wajifanye wanaukagua, je wangesema haufai ingekuwaje?
4. Waandishi wa habari= Wanampa nafasi mno ya kujinadi.
WATAFAKARI.