Hongera sana Mbunge wa Iringa Mjini mchungaji Peter Msigwa

Hongera sana Mbunge wa Iringa Mjini mchungaji Peter Msigwa

kabila01

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2009
Posts
4,235
Reaction score
4,964
Habari zenu wana JF
Leo nimeamua kutoa duku duku langu la kumpongeza mbunge wangu wa Iringa Mjini mheshimiwa mchungaji Peter Msigwa, kwa kuanzisha mashindano ya mpira wa miguu jimboni Iringa yanayojulikana kama Msigwa Cup. Ni wengi wanaanzisha mashindano kama hayo lakini haya aliyoyaanzisha mheshimiwa yameonyesha creativity ya hali ya juu sana wananchi wengi wameyapenda tofauti na walioanzisha wengine waliotangulia. Niliporudi likizo nyumbani Iringa nikakuta mashindano hayo yakiendelea ktk viwanja mbalimbali vya manispaa ya Iringa. Nilichokipenda zaidi ni mashindano kuanzia ktk ngazi ya kata, kila kata ilikua na kituo cha mashindano ambapo timu kutoka kila mtaa zilishiriki na mwisho wa siku kutoa washindi wawili ambao ndo wanaenda kupambana ktk ngazi ya wilaya, nimeshuhudia timu ya viziwi ikisakata kabumbu safi la kuvutia na vipaji vimeonekana. Kila siku jion watu walikua wakifurika kwa wingi sana ktk viwanja mbalimbali kutizama burudani safi ya timu za mtaani. Hongera sana mheshimiwa mbunge.
Kuna mtangazaji mmoja wa kituo cha Redio hapa Iringa nilimsikia akiyapondea sana haya mashindano na kumsifia mbunge wa viti maalumu Ritha kabati kwa kumsapoti kijana mmoja kurekodi wimbo wa mapenzi na mbunge kuweka vocal zake ktk wimbo huu. Mtangazaji huyo anaitwa Edo Bashiri "safi sana Mama kabati kwa kusupport vijana waonekane ktk game sio wengine wanasupport mipira ya miguu ambayo watu wanaishia kupigana ngumi" alinikera sana mtangazaji huyo wadau naomba CV ya huyu mtangazaji inawezekana njaa zikaidharirisha taaluma yake. Vituo vingine vya redio viwe vinaangalia watangazaji wa kuwaajiri huyu nadhani alikua mpiga debe standi akachukuliwa kutangaza ndo maana anaropoka ropoka tu bila ku reason. Hongera sana mheshimiwa mbunge daima mbele usikate tamaa tunataka maendeleo kwa kila sekta ikiwemo michezo

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom