30/03/2016 ndio siku uliyofanya semina elekezi pale Turiani sekondari kwa wanafunzi wa shule mbalimbali za Sekondari, juu ya ugonjwa wa Endometriosis ambao umekutesa kwa muda mrefu sana
.
.Kikubwa ninachokikumbuka ni jinsi ulivyokuwa ukielezea madhara yanayotokana na ugonjwa huu ni pamoja na kuweza kusababisha ugumba, na hapa ndipo ulipokuwa ukitoa machozi kwa kusikitika kuwa hutaweza kuitwa mama.
Lakini leo hii tunazungumza tofauti, sasa unaitwa mama KAIRO, umeonesha dunia kuwa Mungu ndiye muamuzi wa mwisho, tusiache wala kuchoka kumuomba.
Hongera sana dear Millen Magesa