Hongera sana Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, kiongozi bora uliyefanikisha kwa mafanikio makubwa majukumu uliyokabidhiwa ulipoingia madarakani 2024

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wadau hamjamboni nyote?

Haya ni maoni yangu binafsi kwa Rais wa Iran

Naamini anakubalika na wote kuanzia mashariki hadi magharibi, kaskazini hadi kusini!

Mwenyezi Mungu azidi kumpa hekima, ulinzi pamoja na weledi ili kusudi afanikishe kikamilifu malengo yanayotokana na majukumu halisi uliyokabidhiwa

Kwangu Mimi wewe ndiye chaguo Bora na sahihi kabisa kuongoza taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran


Niwatakie usiku mwema
 

Attachments

  • Masoud_Pezeshkian_2024_(cropped)_(2).jpg
    53 KB · Views: 5
Sio undercover kweli huyu? Misimamo yake kama haieleweki eleweki; inapishana na Ayatollah's to some extent.
Kwani huyu ni rais wa kwanza kuwa tofauti kimtazamo na Ayatullah ?
Labda kama ww ni mgeni wa siasa za Iran.
Hasan Rohan alisha wahi kutofautiana sana Ayatollah kuhusu mkataba wa nyukilia mwaka 2015 lakini mwisho wa siku Ayatollah Ali lazimika kufuata maamuzi ya rais na bunge na kukubali kusaini mkataba wa nyukilia.
 
Una uhakika anajua kiswahili? 😀
Anaweza kuwepo hapa JF?
Hivi Kuna uwezekano kule Iran nao wanafuatilia mambo ya Tanganyika🤔😃
 
Jamaa amegoma Kusaini sheria ya mavazi. Wengi walimchagua kwa sababu yeye Hana misimamo mikali ya kidini.
 
Iran ikipata kiongozi mwenye hekima, wananchi wake wataishi maisha mazuri, ya furaha na amani. Wana utajiri mkubwa wa mafuta, lakini wananchi wake wananishi kwenye umaskini na ugandamizaji mkubwa wa uhuru na haki za, huku Serikali ikitumia sehemu kubwa ya mapato yake kufadhili magaidi na kutengeneza makombora, na nchi ikiwa chini ya vikwazo vya kiuchumi.

Fikiria kwa utajiri wa mafuta wa Iran, halafu 30% ya watu wake wanaishi kwenye umaskini mbaya kupindukia, sawa na wa kwetu Tanzania!!
Poverty in Iran has been increasing in recent years:

  • Poverty rate
    In 2023, the poverty rate in Iran was 30.1%, up 0.4 percentage points from 2022. This means that more than 26 million Iranians live below the poverty line.
 
Shia sio Waislam na kama huamini kawaulize Sunni.

Huyo Raisi alichofanikiwa kukataa mara kwa mara kutaka vita na Israel walikuwa hawamuani ile Israel alichowafanya wameanza kumuamini raisi wao.. Aliwaambia kuwa Vita mwishowe ni hasara tu.. Iran ipo sawa ikipigana itapoteza Mafuta Nuclear power infrastructure na uhai wa roho zisizo na hatia.. eti vita ili uonekane mbabe it's stupid. Labda uchokozwe haswa
 
Ww mjaa makamasi kichwani kabla ya kuomba uongozi wenye akili ndani ya Iran kwa nini usiuombe kwenye nchi yako iliyo jaa umasikini na kila aina ya takataka?

Ww mtawaliwa wa ccm una nini cha kuwashauli wairan?
 
Ww mjaa makamasi kichwani kabla ya kuomba uongozi wenye akili ndani ya Iran kwa nini usiuombe kwenye nchi yako iliyo jaa umasikini na kila aina ya takataka?

Ww mtawaliwa wa ccm una nini cha kuwashauli wairan?
Mimi huwa najadiliana na watu wenye akili timamu tu, siyo watu waropokaji, bali wale wanaoweza kujenga hoja, na wenye upeo mpana wa uelewa kwenye jambo linalojadiliwa. Wewe tafuta wa viwango vyako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…