Roho yangu ni ngumu kuliko ninavyoweza kuielezea. haswa kwa masuala yanayohusu nchi yangu Tanzania. couse nilijua siku njingi kuwa tanzania ndiye mama yangu mpendwa, na sikupenda abadan kuikosea ama mtu aikosee nikiwa hai.Yametokea mengi sana ktk nchi hii mabaya na kila mtu mwenye akili timamu ameyajua. but, nijuavyo mimi kila kitu kibaya cha muda mrefu, lazima kinakuwaga na misingi mibaya iliyojengwa kwa muda mrefu.na kuking'oa inahitaji muda mrefu sana, na tena kinahitaji umakini mkubwa na roho ngumu sana.
Nafurahi sana na furaha isiyo na kifani leo hii kwa kutambua kwamba Rais wetu tena kuanzia leo nitakuwa namuita mpendwa wetu JAKAYA MRISHO KIKWETE Kuamua kwa moyo wake wa upendo kwa watanzania, kuamua kuwapa Watanzania nchi yao ili waweze kujitawala na kujiamulia mambo yao wenyewe.ki demokrasia. Mungu ambariki na ampe afya na maisha marefu.
Kitendo cha yeye kama raisi, kuruhusu kutungwa kwa KATIBA MPYA jambo hili siyo kitendo kirahisi kama watu wanavyofikiri kwa sababu, ni kwamba tangu tulipopata uhuru mwaka 1961, ni kama bado tulikuwa tunawaliwa bila ya sisi kujua, kwa kuwa kujitawala kwetu ilikuwa ni kwa mujibu wa sheria walizotuwekea wazungu.
Angeweza kwa mamlaka makubwa aliyo nayo kulikataa jambo hili, na hakuna ambaye angejaribu kama siyo kuthubutu kumwuliza kwa nini. lakni kwa upendo na uzalendo mkubwa alionao kwa nchi yake, ameamua rasmi kuutupilia mbali ukoloni.
Binafsi nimekushukuru mno. na najaribu kufikiri pengine hii ndiyo ile ahadi uliyowahi kutuahidi ya kwamba utakuja kufanya jambo ambalo hatutakaa tukusahau. kwa hiyo kama una jambo lingine ni sawa, lakini kwa hili mimi sintokaa nikusahau. MUNGU AKULINDE TENA NA TENA DAIMA