Hongera sana Simba Sports Club lakini its not over until is over

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Mm binafsi matokeo ya jana yameniburudisha kidogo ingawa naamini Simba ingekuwa na ubora ninaoujua mimi, jana ilikuwa na uwezo wa kufuzu bila kuangalia gemu ya leo ya Gwaneng vs Wydad wala mechi ya mwisho.

Benchika bado hajaibadilisha Simba, kiwango bado sio cha kuvutia.Kipindi cha kwanza wengi tuliona mapungufu ndani ya timu na namna formation anayotumia Benchika ilivyo complex.

Babacar Sarr kiukwel bado, mm naamini Awesu Awesu au yule Akaminko au Yahya Zayd wa Azam au Bajana wana uwezo kuliko Babacar.

Babacar anarudisha sana mipira nyuma, haisukumi timu kwenda mbele, haangalii mbele kuna nn, ukimpa mpira anarudisha kwa manula au kwa inonga au kapombe, anakaribisha mashambulizi.

Chama alicheza vzr lkn naona kuna mkakati wa Benchika wa kumpeleka Yanga kiungo huyu fundi wa mpira.

Ngoma ni mzuri ila yuko slow na wakati mwingine ungongoti wake unampa shida.

Kuwachezesha pamoja Kanoute, Ngoma na Babacar ni changamoto kubwa, timu haiendi na ndio maana Pa Omary Jobe alikuwa akicheza rafu tu.

Ntibazonkiza ana mchango mkubwa sana, kama Robertinho alimpanga, akaja Benchika anaendelea naye, mm nisiyesomea ukocha ni nani nimbishie.

Freddy hapana, hapana, uongozi uliingia mkenge kumtema Baleke, ikiwezekana Baleke arudishwe.

Ni afadhali twende na John Bocco Adebayor lkn sio Freddy.Mchovu sana.

Micquisone anapambana sana lkn kiukweli kiwango hakipo, msimu ujao hatunaye.

Simba ingekuwa na akaminko, awesu, Feitoto, ayoub lyanga naamini ingekuwa bora zaidi, ushauri wangu Babacar, Freddy, Pa omary, Kanoute, Micquisone na kwa sababu pia Saido ana pressure ya mashabiki wapeni mkono wa kwaheri, hawana jipya tena.

Professional kama Sadio kanoute unapata chance kama ile unaikosaje?

All in all mungu nipe furaha leo mbuzi wa kijani waliojipaka rangi kama mademu wa baa wafe zozote zile.
 

Bado mnahangaika na haya matimu?

Kwa mfano SSC ikavuka robo fainali;

Unadhan itaenda kokote?

Ni upotezaji wa muda
 
hizi akili mnazitoa wapi hao kina bajana, akaminko,fei,ongeza na dube wameshindwa kufuzu makundi shirikisho kwa kutolewa na katimu kadogo unatarajia waivushe simba robo final club bingwa, tuwe serious jmn
 
Inahitaji moyo wa chuma kuizungumzia Simba inapokuja kwenye suala la usajili kwa kwa misimu hii mitatu/minne uliyopita. Pesa iliyotumika kumsajili Jobe na Freddy kwa pamoja ingetumika tu kumsajili mshambuliaji mmoja hatari anayejua goli kutoka nje na chenji inayobaki isajili mshambuliaji mwingine mmoja wa ndani basi. Uawaacha Phiri na Baleke sawa hawafungi halafu unaleta Jobe na Freddy ambao viwango vyao havipishani na hao ulio waacha sasa ndio kimefanyika kitu gani.

Chama atalaumiwa sana kwa sababu Simba pale mbele hakuna mshambuliaji mwenye jicho la goli. Chama huyu huyu anyeonekana kachoka kwa sababu ya uwezo kupungua kutokana na umri bado akipata timu ambayo ina washambuliaji wazuri amini nawaambieni bado na uwezo wa kufanya makubwa hata misimu mitatu inayokuja. Kila mechi ya Simba Chama lazima atengeneze nafasi kwa washambuliaji zisizopungua mbili za wazi za magoli sasa timu inataka nini tena?

Miquisone alisharudi vizuri kabisa lakini benchi la ufundi limeamua kumpoteza mazima. Aliye karibu na Miquisone amshtue atafute timu nyingine itakayompa nafasi kuokoa kipaji chake kinachopotezwa bure. Mkalimani akifika dakika ya 50 anaanza kuanguka anguka uwanjani halafu mbinafsi kweli kweli hachezi kitimu wakati Miquisone yupo benchi baadae anapewa eti dakika 5 amalizie mpira huo si uzezeta kabisa.

Iwapo Simba jana ingekuwa na na washambuliaji imara basi wangepata ushindi kirahisi sana. Na hili zimwi la safu ya ushambuliaji litawasumbua mpaka mwisho wa misimu kimataifa na hata k wenyeligi ya ndani.
 
hizi akili mnazitoa wapi hao kina bajana, akaminko,fei,ongeza na dube wameshindwa kufuzu makundi shirikisho kwa kutolewa na katimu kadogo unatarajia waivushe simba robo final club bingwa, tuwe serious jmn
Sikia ww hao wachezaji wanacheza azam huwez kuona impact, azam usifananishe na Simba, feitoto alipokuwa yanga na ss hv azam wako sawa, hao wakija simba brand inakuwa kubwa
 
All in all mungu nipe furaha leo mbuzi wa kijani waliojipaka rangi kama mademu wa baa wafe zozote zile.[emoji23]
 
All in all mungu nipe furaha leo mbuzi wa kijani waliojipaka rangi kama mademu wa baa wafe zozote zile.
 
Sikia ww hao wachezaji wanacheza azam huwez kuona impact, azam usifananishe na Simba, feitoto alipokuwa yanga na ss hv azam wako sawa, hao wakija simba brand inakuwa kubwa
Fei ambaye yupo azam takwimu bora sana mpaka sasa magoli 8+ na assists 2+ sio mbaya pengine muda wote aliocheza yanga kwa msimu mmoja akuwahi kupata takwimu hizi
 
Ukiangalia uwezo wa wachezaji wetu wengi wakimataifa upo chini kiukwel yaan chrmalone,inonga kidogo na ayubu anajitahid ila wengine wanaungaunga sana kina chama saido wote hawanauwezo wa kutupa chochote cha maana kuhusu miquissone jamaa anajitahidi kurudisha japo nusu ya uwezo wake lkn miquesson ni mchezaji mzur pale timu inapokuwa inacheza one two nyingi ni mwepesi kutafuta free space tatizo viungo wengi ni wagumu had washambuliaji ungeniambia mimi kati ya chama saido na miquissone abaki nan ntakujibu miquesson sabb huwa anajitahd kuonyesha impact fln kila anapoingia na sio mtu anaetabirika ila saido na chama uchezaji wao ni wakutabirika sana.
Not easy ila fredy,kanoute,chama,onana,saidoo,ngoma wote hawa niwakuacha tu hawawez leta impact kubws mbeleni
 
hizi akili mnazitoa wapi hao kina bajana, akaminko,fei,ongeza na dube wameshindwa kufuzu makundi shirikisho kwa kutolewa na katimu kadogo unatarajia waivushe simba robo final club bingwa, tuwe serious jmn
Aisee! Wewe akili zako Zina Akili kweli! Hongera! Hivi mtu hujiulizi, kama hao wachezaji Wana huo uwezo, walishindwaje kuutumia Ili timu zao zisonge mbele? Miaka yote hii mbona ata hatua ya makundi ya kombe la Washindwa hawafiki!
 
Sawa tumekusikia shabiki wa utopolo majini fc,, popoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…