Mtanange wa leo kati ya Simba na TP mazembe ulikuwa mkali sana na wa kusisimua. Hongera sana Timu ya Simba mchezo mliouonyesha leo hakuna mfano. Mmecheza kwa uelewano mkubwa sana na kwa asilimia mliwazidi wapinzani wenu na hasa kipindi cha pili. Sifa kem kem ziwaendee Mohamed Hussein, Chama, Nyonzima, Kagere na wachezaji wengine wote. Kwa kweli mmetufurahisha. Msihofu japo tumekosa goli lililogonga mwamba na penati. Huo ndiyo mchezo. Tujipange kwa hatua ya marudiano.