Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
Poleni kwetu sote juu ya kuondokewa na Mzee wetu John Magufuli, kifo ni kifo na kamwe hakizoeleki.
Napenda kuwashukuru sana Wafuasi na Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa maneno ya busara hasa katika kipindi hiki cha msiba, naomba nieleweke kuwa wenzetu wa CCM wasingeweza kuwa na ustahimilivu hata punje jambo kama hili lingetokea upande wa CHADEMA.
KWA MFANO
Mali za Mbowe zilipoharibiwa hakuna mwana CCM aliyehuzunika wala kukemea jambo lile, Lissu aliposhambuliwa kwa risasi mchana kweupe, aliitwa msaliti, nakumbuka Mwenyekiti wa CCM Iringa (sina uhakika) aliwahi kurekodiwa akihamasisha "kumalizwa kwa wasaliti", Lowasa alitukanwa kila aina ya tusi, Lissu aliitwa, ameitwa na anaendelea kuitwa SHOGA na wana CCM na hakuna anayekemea, Mawazo inasadikika aliuwawa mchana kweupe na watu waliosadikika kuwa wafuasi wa CCM, hakuna mwana CCM hata mmoja alipaza sauti.
Ni mengi ya kuelezea, pengine kwa mtazamo wangu, CHADEMA wangeweza kuitumia hii fursa kulipiza kisasi ila kwa hakika wametoa pole na wote tumekuwa kitu kimoja. Niwashukuru sana na msiba huu wa Mzee Magufuli utumike kuwa CHACHU ya kutuunganisha na kuijienga Tanzania. Tujiponye na kuanza upya, hatujachelewa.
Nitamkumbuka Magufuli kwa kukataa hotel ya SUGU Mbeya isibomolewe kwa visa tu vya kisiasa.
Pumzika kwa amani John