Tanzania tumekua na timu nzuri sana za vijana, Serengeti boys na hata Ngorongoro heroes. Kuna ile timu iliyoenda Brazil na kuchukua kombe lakini ilivyorudi iliachwa na hadi leo wengi wao wako mtaani(mchangani).
Kutokana na hali hiyo ningependa kuona vijana hawa was Serengeti boys hakipotei tena. Hivyo ningeshauri ziwekwe Sera na sheria zitakazovitaka vilabu vya ligi kuu kuwachukua vijana hawa katika vilabu vyao Ili wasipotee. Sambamba na hilo TFF itenge fungi maalam kwa ajili ya posho zao ikishirikiana na serikali.
Mwisho;Hongera Serengeti boys.