mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Ni mbumbumbu tu anayeweza kuamini kuwa usaili ndio wenye uwezo wa kutupatia walimu bora!! Usaili unasaidia tu kuondoa wengine na kubakiza wachache kulingana na nafasi zilizopo!! Utaratibu wa usaili haufai kabisa kwa taaluma ya ualimu na afya.
Utaratibu wa zamani wa TAMISEMI kuwapangia walimu na watumishi wa afya vituo vya kazi kwa utaratibu wa FOLENI huo ndio unaofaa!! Kila aliyehitimu anafaa!! kama hafai kutokufaa kwake hakuwezi kugundulika kwa usaili!!
Inabidi tuviamini vyuo vilivyowafundisha na kuwatunukia vyeti vya kuhitimu!! Daktari asomee taaluma yake kwa miaka 6 kisha bodi yake ikampima na kumpatia leseni, halafu anakuja mtu anadai anaweza kupima ubora wa daktari huyu kupitia usaili wa dakika chache tu kwa siku moja! (haya ni matusi).
Hali kadhalika kwa walimu!!
Ndiyo maana watu wengi wameipongeza serikali kwa sitisho hilo wakiamini kuwa utaratibu wa zamani utarudishwa!! Kuwafanyisha usaili walimu walio malaki ni uharibifu wa rasilimali fedha na muda!!