Leo Serikali imetoa waraka mrefu unaoelezea namna Watanzania wanavyotakiwa kupambana na tatizo la Covid 19. Kiufupi mwongozo huo wa Wizara ya Afya, unaoelezea zaidi mambo yanayotakiwa kufanywa ili kupunguza maambukizi, wajibu wa mamlaka mbalimbali za usimamizi, na wajibu wa kila raia.
Mapungufu makubwa katika waraka huo ni kutoelezea kwa kina ukubwa wa tatizo, na namna tutakavyofanya monitoring ili kujua Kama tunafanikiwa au hatufanikiwi. Lakini pia kuna maneno mengi ya kuzungukazunguka, ambayo hayakuwa na umuhimu wowote. Muungwana angekuwa straight kwenye tatizo kubwa la sasa, ambalo ni Covid 19. Hadithi nyingine hazina maana.
Mafanikio ya kitu chochote, hupimwa kwa tafiti na data. Ni vema sasa, Serikali iruhusu kufanya upimaji, angalao kwa kuanzia na wale wagonjwa wote waliopo hospitalini. Hii itawasaidia matabibu wetu kuwa na uhakika na aina ya magonjwa wanayoyatibu. Daktari unapomweleza tatizo lako la afya kwa namna unavyojisikia, huorodhesha vipimo vinavyotakiwa kufanywa, lakini kwa sasa kutokana na misimamo mbaya uliokuwepo wa Serikali, daktari anaandika vipimo vyote lakini anaogopa kuandika Covid 19 test. Hii kasoro iondolewe Mara moja.
Mimi ni kati ya watu waliokuwa wamemdharau kabisa huyu Waziri wa Afya, na kujiuliza maswali mengi aliwezaje kuupata huo udaktari kutokana na matamko yake ya awali.
Waraka wake wa sasa, ukilisoma, ukiambiwa umetolewa na Waziri daktari wa afya, huwi na shaka, japo bado umekosa ujasiri wa kitaaluma.
Kuna watu, ambao ni viongozi wamefanya makosa mengi katika kukabiliana na ugonjwa huu wa corona. Lakini maadamu sasa wanakiri kukosea kwa kubadilisha kauli zao, wote tuungane na kumkabili adui yetu wa pamoja.
Hongera sana wote mliopiga kelele dhidi ya mapungufu ya Serikali katika kukabiliana na Covid 19. Shukrani nyingi kwa WanaJF wale wenye akili timamu na dhamira njema (ukiondoa ukiondoa wachache wanaoamini wanatakiwa kuitetea Serikali kwa kila kitu - ambao humu JF wanajulikana kwa jina Mataga), hongereni Maaskotu, hongera sana Baba Askofu Mkuu Jimbo Kuu Katoliki Dar, hongera shekhe Ponda, Hongera Askofu wa Lulenge, Hongera kwangu pia maana nami ni kati ya waliopandisha mada nyingi dhidi ya corona. Ni hizi sauti, naamini zimechangia katika kuifanya Serikali kujitafakari katika Yale ambayo ilikuwa ikiyafanya.
Narudia tena, mataga mjitafakari sana, kuona kama kweli ninyi ni watu wenye akili timamu. TWAWEZA kwenye utafiti wao, walibaini kuwa CCM inapendwa zaidi na watu wajinga, na kwenye mijadala mingi hapa jukwaani, imedhihirika hivyo. Wametudhihaki sana tuliokuwa tukiitaka Serikali kuchukua hatua, kutoa mwongozo, na kuelekeza usimamizi wake. Lakini mlitudhihaki, mlitutukana na kutukejeli sana. Sasa Serikali imeyachukua mawazo yetu, na inaenda kuyasimamia. Ninyi mtaendelea na misimamo yenu hasi ya kuona kuvaa barakoa, kuwapima watu, kupunguza misongamano, ni ujinga?
Mataga acheni ushabiki kwenye mambo ya msingi. Mnapofanya ujinga kushabikia ujinga hammsaidii Rais, hamuisaidii Serikali, hamuisaidii CCM wala Taifa hili kwa ujumla. Mambo ya kijinga mnayoshabikia, ndiyo yanayowafanya watu wenye akili kubwa na wasiopenda ushabiki, kujitenga na CCM.
Tujipe pole tuliondokewa na wapendwa wetu kutokana na Covid 19, huenda kungekuwa na tahadhari mapema dhidi ya ugonjwa huu, tungeokoa maisha ya baadhi ya marehemu. Makosa yaliyofanyika, hata tukafika hapa ambapo ni misiba kila sehemu, yatujenge katika kuhakikisha makosa ya namna hii hayatokee tena siku za mbeleni.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu wajalie ufahamu Watanzania ili wakati wote wapiganie kuwapata viongozi wa kuwaokoa badala ya kuwaangamiza.
Waraka wa Serikali huu hapa:
www.jamiiforums.com

Waziri wa Afya: Epukeni misongamano isiyo ya lazima, vaeni barakoa safi na salama
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO TAARIFA KWA UMMA TAMKO LA KUONGEZA KASI YA UTEKELEZAJI WA HATUA ZA KUJIKINGA NA MAGONJWA YA KUAMBUKIZA NA YASIYOAMBUKIZA NCHINI Dodoma, Jumatano 24 Februari, 2021. Ndugu Wananchi, kila mwaka kipindi...