#COVID19 Hongera Serikali kwa Mwongozo wa Kupambana na Covid 19

Mafanikio ya kitu chochote, hupimwa kwa tafiti na data. Ni vema sasa, Serikali iruhusu kufanya upimaji, angalao kwa kuanzia na wale wagonjwa wote waliopo hospitalini
Kwahiyo hata walio hospital hawapimwi‼️⁉️; kiongozi. Hata kama unajambo lako- kwahili nakushauri uongee ukweli, ukiongea ukweli hupati hasara yoyote na ukiongea uongo hupati faida yoyote
 
Unataka uishi mpaka lini mzee? Sisi ni wasafiri bwana mkubwa, wakati ukifika lazima twende, kuna magonjwa hatari zaidi ya corona, umewahi kuona ama kumwuguza mgonjwa wa TB??? Corona ni vita ya kiuchumi..
Hivi kuna mgonjwa analazimishwa dawa na chanjo??? Ziko nchi ngapi dunia kwanini wanakomaa sana na TZ? maanake hapa ndio tunakufa kuliko marekani?
 
Well done
 
Ni sawa na kukumbuka shuka asubuhi. Wananchi wamezidi kupotea maisha
 
Acha uwongo, mtu mzimaaa!
Waziri amesema kujinga na changamoto ya kupumua na magonjwa ya kuambukiza siyo corona

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Mwenzenu kadungwa chanjo nyie endeleeni kujifukiza
 
Baada ya tahadhari na kuchukua hatua bado mapambano na kirusi yanaendelea duniani kote. Wataalamu wanadai ili kutokomeza COVID 19 dunia nzima iwe imepata chanjo mapema maana kirusi kikiachwa kitawale eneo fulani kina tabia ya kujibadilisha kiendelee kuishi. Haya yameonekana katika sehemu ambazo kiliachwa kisambae kama uingereza,brazil na afrika kusini, kikiendelea kuishi maana yake ni vifo kwa binadamu.Ilichukua miaka 184 kutokomeza ndui. Bila dunia kuwa na umoja katika mapambano kirusi hiki kitatawala dunia.
 
Hili ulilolisema ndiyo hofu kubwa ya Dunia. Huu siyo ugonjwa ambao unaweza kusema kila nchi iamue kama watu wake wachanjwe au la. Kwa sababu ugonjwa kuendelea kuwepo sehemu moja ya Dunia ni kuacha uendelee Dunia nzima.

Mutations ya virus italazimisha kutafiti chanjo nyingine. Waliochanjwa wote itabidi wachanjwe tena, na pengine ikawa ngumu zaidi kupata chanjo itakayofanya kazi vizuri.
 
Hongera Askofu wa Lulenge, Hongera kwangu pia maana nami ni kati ya waliopandisha mada nyingi dhidi ya corona. Ni hizi sauti, naamini zimechangia katika kuifanya Serikali kujitafakari katika Yale ambayo ilikuwa ikiyafanya.
Usisahau kuwataja
UDSM, SUA, OUT, etc
 
Mimi ni kati ya watu waliokuwa wamemdharau kabisa huyu Waziri wa Afya, na kujiuliza maswali mengi aliwezaje kuupata huo udaktari kutokana na matamko yake ya awali.
Huyu nimemfuta kabisa kwenye professionalism
 
Nawapongeza kwa kuacha utoto , siku nyingine wasisubiri mpaka Corona iwachukue watu wao wa karibu ndio wachukue hatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…