Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Kwa muda mrefu sana, Maendeleo ya Tanzania yamekuwa yakirudishwa nyuma na mambo mbalimbali ikiwemo
1. Hujuma kutoka mataifa jirani
2. Hujuma za wafanyabiashara wakubwa
3. Ujinga wa Watanzania
Kusema ukweli tangu nimeanza kupata akili nimesikia mipango mingi sana ya nchi yetu ambayo mwisho ilikuja kutofanyika kabisa kutoka na moja ya sababu nilizozitaja hapo juu.
Tangu Serikali ya Awamu ya 6 iingie madarakani moja ya kitu ambacho nawasifu ni kuwa focused kwenye malengo na kutoendeshwa na haya mambo matatu niliyoyataja.
Mfano mzuri ni hili jambo la Bandari.
Washindani wetu walijipanga kweli kuharibu huu mpango wa kuifanyia maboresho makubwa Bandari yetu ila kusema kweli kwa namna Serikali ilivyoweza kusimama kwenye hili napenda kusema kwa dhati! Nimevutiwa sana!
Moja wa watu waliokuwa na mipango mikubwa na ya maana alikuwa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete ila alishindwa pakubwa sana na hujuma za majirani pamoja na matajiri hadi mipango yake mingi ya kuibadilisha Tanzania ilikuja kuhujumiwa na majirani na kuishia kwenye makaratasi tu.
Kikwete angesimama, leo Kingamoni ingekuwa Mini Dubai na tungekuwa na watalii wengi sana wanaokuja kula bata tu Kigamboni na kuingiza fedha za kigeni za kutosha. Ila kwa hujuma mipango ile iliharibiwa na watu wakapaste na kuanza kujenza Konza Satellite City nchini kwao.
Leo Kikwete angesimama, Dar lingekuwa Jiji la kipekee na kuingiza uchumi mkubwa sana ila mipango mingi iliharibiwa na moja ya makundi hapo Juu.
Ili Tanzania irate maendeleo ya kweli lazima vyombo vyetu vya Ulinzi vifungue macho na kuwekeza zaidi katika kusoma mwenendo wa Dunia na majirani.
Kwa bahati mbaya eneo hili tulipwaya sana hivyo kupelekea kuhujumiwa sana. Ila kusema kweli kwa mwendo wa awamu ya sita. Napenda kusema hongera sana Rais Samia. Wewe ni jembe kweli!
Huko Uingereza Taasisi zao za Ujasusi zimeweza hadi kujua namna washindani wanavyozingilia nchi yao ili kuwahujumu. Kwa sasa Tanzania tumeanza kwenda vizuri ila tusirudi nyuma! Mwendo uwe huu huu