Hongera Simbachawene na Utumishi, lakini ni sahihi kwa watumishi wa umma wawapo kazini kuwa na mavazi yenye nembo au picha za watu fulani?

Hongera Simbachawene na Utumishi, lakini ni sahihi kwa watumishi wa umma wawapo kazini kuwa na mavazi yenye nembo au picha za watu fulani?

Mwanagenzi

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2006
Posts
738
Reaction score
273
Leo nimekusikiliza ukiongea kwenye kikao kazi cha wakuu wa taasisi za umma Dodoma. Umeongea mambo mengi mazuri, makubwa na ya msingi kwenye hotuba yako ya ufunguzi. Umezungumzia changamoto mbalimbali za kiutumishi, uwajibikaji, maadili nk. Umetoa mifano hai na ufafanuzi wa kueleweka. Nakupa kongole.

Nina jambo moja linalonitatiza: ni sahihi kwa watumishi wa umma wawapo kazini kuwa na mavazi yenye nembo au picha za watu fulani? Kwa mfano mtumishi kuvaa beji yenye picha ya rais, au jina lake, siyo aina ya hongo au rushwa kwa mamlaka ya uteuzi?

Nikiwa mtaani nimevaa nembo hizo nadhani ni sawa maana si mahali pa ofisi ya umma. Ni kuonyesha hisia zangu za kumhusudu huyo niliyemvaa.

Je, Mtumishi anaweza kuvaa beji au kofia yenye picha ya Waziri wake au Mkurugenzi wake?
.
 
Back
Top Bottom