Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Gazeti: Uhuru
NA SULEIMAN JONGO
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, jana alizindua mradi wa kuendeleza sayansi katika vyuo vikuu, na taasisi za elimu ya juu wenye thamani ya sh. bilioni 130.
Akizindua mradi huo mjini Dar es Salaam, Profesa Maghembe, alisema hiyo ni hatua moja ya kuendeleza sekta ya sayansi na kuongeza wataalamu.
Mradi huo, unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, utakuwa na awamu tatu ambapo mbili, kila moja itakuwa na gharama hiyo.
Profesa Maghembe, alisema mradi huo utawezesha ununuzi vifaa vipya katika vyuo vikuu vya umma, kuvipanua, kuongeza idadi ya wanafunzi na kuwaendeleza wahadhari wasaidizi kitaaluma.
Alisema katika mazingira ya maendeleo ya teknolojia duniani,nchi haiwezi kuendelea kisayansi kama haitakuwa na vifaa vya kisasa vitakavyoweza kutumika kwa mafunzo ya vitendo.
"Kuna baadhi ya vyuo nilipovitembelea nilikutana na vifaa ambavyo mimi mwenyewe nilifanyia utafiti wakati nafanya shahada yangu ya udaktari wa falsafa katika miaka ya 1970, sasa unaweza kuona ni jinsi gani tulivyokuwa na matatizo," alisema.
Kaimu Meneja wa Benki ya Dunia nchini, Chiyo Kanda, alisema ufadhili huo umekuja kwa kuthamini juhudi za Tanzania katika kuendeleza sekta ya elimu.
Chiyo alisema kuanzia miaka ya 2000, Tanzania imekuwa ikifanya vyema katika sekta ya elimu, huku idadi ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya sekondari ikiongezeka sambamba na wale wanaojiunga na vyuo vikuu na taasisi za elimu za juu.
Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, Profesa John Kondoro, alisema mradi huo utawezesha kuinua kiwango cha teknolojia nchini.
Profesa Kondoro alisema, kutokana na uhaba wa kifedha baadhi ya kozi zilikuwa zilishindikana kuanzishwa, sasa itakuwa ni rahisi kufanya hivi.
My Take:
Now lets make the safeguards and benchmarks za kutuonesha kuwa hizo bilioni nyingi haziishii kununua vifaa vya ajabu ajabu. Watuambie tutapima vipi maendeleo yetu ya Sayansi na Teknolojia tukiwa na msaada wa aina hii. Hii ndiyo misaada ninayoizungumzia mimi. Misaada ya kuwezeshwa kuwa huru siyo kudekezwa kuwa dependent.