Hongera Suleiman Nyambui kwa Kuteuliwa kuwa Kocha Mkuu Brunei

Governor of Bettors-GB

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2013
Posts
10,568
Reaction score
9,710
Nachukua nafasi hii kumpongeza Suleiman Nyambui kwa kuchaguliwa kuwa Kocha wa Team ya Riadha ya Taifa ya Brunei.

Nimefuatilia Maelezo yako AZAM Tv na nitafuatilia Jpili hii utapokuwa Live na Charles Hillary kama mlivyoahidi AZAM tv ili kujua undani zaidi.Ila msituzingue kama hao mnaowaalika kwenye Siasa wanakimbia.Tuleteeni Nyambui bila kubadili ratiba.Maana nasikia Nyambui wiki ijayo anakwe pipa

Kweli Taifa letu limelala,yaani hadi nchi ya Nje ndio inaona thamani ya Kocha wa ndani.
Nimechovutiwa zaidi
-Uliombwa kwa Mkataba wa Miaka miwili,ukagoma,na kusema kwamba wakupe miezi sita ili uangalie kama Nchi yenyewe inataratibu na plan nzuri na utashi wa kuendeleza Riadha.
Hii ilinivutia saaana,maana hukufanya tamaaa,na ninajua umejifunza hapa Tanzania.Maana Tanzania tunapenda sana michezo na ahadi za mezani,ila dhamira zetu mioyoni kama Taifa ni ZEROOO,tena nasisitiza ZEROOOOO.Hasa kwenye Riadha ndio kabisaaa.
Na hata hivyo nakupongeza sana kwa uvumilivu wako hapa Tanzania,umetoa mchango mkubwa sana na sie kama wadau wa Riadha tumeona Juhudi zako kwa miaka Mingi saaana.Na lazime niwe mkweli,una moyo wa chuma aisee.Maana kama mie nisingeweza,ningeachia njiani.Umesimamia mchezo huo bila malengo yako kutimia kwa kukosa ruzuku Serikalini na wadhamini wa uhakika.Na pia umegundua kabisa kwamba Serikali haina mkazo kwenye riadha.
Umekuwa Ukishauri Serikali na wadau mara kadhaa juu ya ju invest kwenye huu mchezo bila mafanikio,na wala huku kata tamaa mpaka leo.

-Sie wadau tunakutakia kila la Kheri huko uendako,mungu akusimamie na ufanikiwe.

Angalizo:-
Nakuomba ukiitwa Tena Tanzania usije,sie Watanzania tuna tabai ya kudharau cha kwetu.Na pindi mtu akipata mafanikio nje ya basi tunajifanya ndio kuweka mipango telee,na mtu akija hakuna lolote.
Aliletwa Kocha M Cuba kwenye ngumi,leo ngumi zipo wapi ,hovyoo tu.
Kuna Mchezaji kama sikosei yupo Chelsea B,alipitia kwa msaada wa Chama cha soka Kenya ndio alifanikiwa kuombewa majaribo wakati huo TFF walikataa kumpa na kumkebehi saaana kwamba wewe hata Ligi kuu haumo utaitwaje Ulaya.

Nakushauri jitahi sana ufanye vizuri.Na pia tafuta hata Private runner akuajiri ili umsimamie.
Lakini hapa kwetu Tanzania usifundishe tena,utajiharibia CV yako bureee.Serikali haina mpango wowote wa kuinua na kuendeleza Riadha.Wanasubiria ufe tu ndio ujue jinsi watu wanavyosifia umahiri wako na mipango yako ya Siasa.
Mfano wa Hotuba:(Samahani kama Nyambui utakwazika,ial ni unchungu wa jinsi nchi haijali huu mchezo)
Waziri wa Michezo akisoma wasifu wa Marehem
Ndugu Marehem Nyambui alituletea sifa kubwa saana kwenye Mchezo wa riadha kwa kutuletea medali mbili kubwa.

Marehem alikuwa mpenda watu saana,na alieamua kuhama Marekani na kuja kuendeleza Riadha hapa kwetu.Na mara ya mwisho kukutana alikuwa ameleta wizarani progam yake mpya ya michezo mashuleni.Na hii kwa serikali kuthamini mchango wake tumeishaianza muda mrefu uliopita(uongo),na ndio maana tumeanza kwenye umiseta(uongo square).
Na tunaahidi kwamba juhudi zake na mipango yake ya kuendeleza riadha itaendelezwa.
Mungu ailaze roho ya marehem mahala pema peponi,huku kimoyoyo akimalizia kwa kusema na Mungu aulaze Mchezo wa Riadha kuzimu

NYAMBUI TUNAKUOMBEA KWA HESHIMA UMEOPEWA NCHI YA BRUNEI


===================
===================


 
Yaani ni kitu ukweli lakini na yeye alikuwa mlaji mzuri wa pesa za kuendeleza riadha tz
 
Mfano wa Hotuba: (Samahani kama Nyambui
utakwazika,ial ni unchungu wa jinsi nchi haijali
huu mchezo)
Waziri wa Michezo akisoma wasifu wa
Marehem
Ndugu Marehem Nyambui alituletea sifa kubwa
saana kwenye Mchezo wa riadha kwa kutuletea
medali mbili kubwa.
Marehem alikuwa mpenda watu saana,na
alieamua kuhama Marekani na kuja kuendeleza
Riadha hapa kwetu.Na mara ya mwisho
kukutana alikuwa ameleta wizarani progam
yake mpya ya michezo mashuleni.Na hii kwa
serikali kuthamini mchango wake tumeishaianza
muda mrefu uliopita(uongo),na ndio maana
tumeanza kwenye umiseta(uongo square).
Na tunaahidi kwamba juhudi zake na mipango
yake ya kuendeleza riadha itaendelezwa.
Mungu ailaze roho ya marehem mahala pema
peponi,huku kimoyoyo akimalizia kwa kusema
na Mungu aulaze Mchezo wa Riadha kuzim.
Teh,teh,teh, hyo mistari ndo imeniongezea seconds za kuishi coz watz kwa unafiki hatari sana
 
mtoa mada inawekana haujui unachokiongelea hapa
huyo nyambui amekuwa katibu mkuu wa riadha Tanzania labda ungetueleza yeye kama kiongozi amefanya nini katika maendeleo ya mchezo wa riadha. amefanya training ngapi za makocha? ameandaa mashindano mangapi ya kitaifa au kimataifa nchini? amefanya juhudi gani kuhamsisha watu wengi kushiriki kwenye riadha au ametumia vipi hela wanazopekewa kutoka shirikisho la mchezo wa riadha duniani.
ukipata hayo majibu ndipo utaelewa unamuongelea mtu wa namna gani hapo
 

We ndio hujuii kabisaa.
Sasa na wewe Uliza Wizara ya inayohusika na Michezo kwamba ilikuwa inatenga fungu kiasi gani kwa upande huo ndio utajua.
Wewe unafikii yeye malaika,atoe pesa mbinguni ndio afanye unayotaka wewe.
Nyie ndio meofanya team ya taifa ifeli kwa kubahatisha.Kumbe bado mpo alive?Nchi kweli imekwisha
 
Mshindi wa zamani wa medali ya fedha ya michuano ya Olimpiki, Suleiman Nyambui amepata kazi ya kuwa kocha mkuu wa Brunei.

Nyambui, aliyeshinda medali ya Olimpiki mwaka 1980 wakati wa michuano ya Olimpiki ya majira ya joto nchini Moscow,amesema kuwa amepewa mkataba wa kuifundisha timu ya taifa ya nchi hiyo kwa miaka miwili, ila atafanya kazi kwa miezi sita kuangalia mazingira.

"Wameniomba kuwa kocha kwa miaka miwili, nami nimewaomba, kwa kuanzania, kufundisha kwa miezi sita ili nione mazingira, baada ya hapo huenda nikabaki", alisema Nyambui.

Nyambui, ambaye amesema atajiuzulu nafasi yake ya ukatibu mkuu wa chama cha Riadha Tanzania (AT), aliwahi katika miaka ya nyuma kuwa kocha nchini Marekani, visiwa vya Bahrain na alipata kufundisha nchini Australia mara kadhaa kwa mikataba ya muda mfupi mfupi.

Nyambui amesema anategemewa kuondoka Dar es Salaam kuelekea Brunei kuanza majukumu mapya.

Chanzo: http://www.bbc.com/swahili/michezo/2015/06/150621_nyambui_coach_brunei
 
Hongera zake, akajitahidi kazi yake iwe na matokeo mazuri ili kazi iendelee. Huko hakuna visingizio. Kila la heri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…