Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Naamini ujio wa Sungusia TLS utaendeleza harakati na vuguvugu la kuirudisha TLS kuwa chombo cha kitaaluma chenye nguvu na hari ya kusukuma utawala wa sheria.
Kitarudi kuwa chombo kinachotazamwa na watu kama njia ya kufikia haki pamoja na chimbuko la mawazo mapya. Kitakuwa chombo chakusukuma mbele katiba ya wananchi na siyo katiba ya wanasiasa. Kitakuwa chombo cha kushauri vyema bunge, serikali na mahakama na siyo chombo kilichojichimbia Ikulu.
Chama kimerudi kwa wanachama; nakumbuka katika kukivunja nguvu chama hiki Palamagamba alikigawa kwa kuwaondoa mawakili wote walioajiriwa serikalini na kuwatengenezea chama chao na hivyo leo hii kuna TLS na chama cha wanasheria wa serikali. Vyote vilikuwa domant lakini sasa naamini kimoja (TLS) inakwenda kujinasua mikononi mwa akina Kaburi wasiowaza kuhuru wa taaluma.
Karibu TLS ukitambua unayo kazi kubwa mbele yako yakuwaaminisha watu kwamba ni chama cha kuwatetea na kuwasimamia Watanzania.