Mtukudzi
Senior Member
- Nov 14, 2013
- 103
- 408
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!
Naipongeza mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) kwa mabadiliko makubwa mliyofanya kiasi cha kuifanya mamlaka kuwa rafiki badala ya kuwa adui kwa walipa kodi. Binafsi nimeona mabadiliko haya chanya kuanzia January 2021. Wafanyakazi wa Mamlaka hii wamekuwa wasikivu na wamekuwa watu waelewa sana kulinganisha na miaka ya nyuma tangu kuanza kwa utawala huu wa awamu ya tano.
Kisiasa, hii inamuweka juu Mh. Magufuli kwa sababu karata aliyoicheza ya kumpa Bw. Mwambe nafasi ya uwaziri wa viwanda kwa namna moja au nyingine imeleta tija kwa njia isiyoweza kuwa wazi.
Kabla ya uwaziri, Bw. Mwambe alikemea tabia mbaya ya TRA akiwa TIC. Naona baada ya kuingia kwenye Baraza la Mawaziri ametema nyongo na sasa matunda yanaanza kuonekana.
Rai yangu ni kuwa TRA endeleeni na spirit hii. Hata watu waliokimbiza mitaji yao nje watairejesha muda si mrefu.
Hongera TRA, hongera Waziri Mwambe, hongera Rais Magufuli.