Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nikipata fursa, huja na makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa"
Hili ni maslahi ya taifa ya pongezi kwa TRL, nimeona mzigo wa mabehewa mapya ya kisasa ya reli ya kisasa ya SGR ukipokelewa bandarini, DSM, hivyo hatua ya kwanza ni kutoa pongezi kwa TRL
Tulichoelezwa ni hiki
Kwa sisi baadhi yenu, tulioishi nchi za wenzetu, tumepanda treni hizi za kisasa za kasi zinazoendeshwa kwa umeme, bulet trains, ambazo zinakwenda hadi kasi ya speed 160kmh kwa saa!, ila mabehewa ya abiria ya wenzetu tuliyo yapanda, sio kama haya tunayo letewa sisi!, hivyo kwanza natoa hongera sana TRL kwa mabehewa haya.
Kwavile SGR ni reli mpya ya kisasa, je vichwa, mabehewa haya tulioletewa ni mabehewa mapya ya kisasa? Kwa jicho tuu la kawaida, behewa hilo ni lile la kwenda mwendo kasi wa 160kmh?. Naona kama sio! Kama tumenunua mabehewa mitumba, tuelezwe tuu, Watanzania ni watumiaji wazuri wa vifaa used, na hakuna ubaya wowote kutumia vitu vilivyotumika yaani used au mitumba, Ila kitu muhimu ni kwa Watanzania tuelezwe tu ukweli kuwa mabehewa haya ni used, na sio viongozi wetu watueleze tumenunua mabehewa mapya ya kisasa, kumbe ni mabehewa mitumba yaliyo karabatiwa, kupakwa rangi na kufanyiwa nakshi nakshi tu?
Hapa ninachokisoma na kinachokanushwa ni vitu viwili tofauti, kwanza Watanzania tunapaswa kuambiwa ukweli
1. Taarifa ya TRC inasema vichwa vipya na mabehewa mapya, lakini ukweli ni kuwa ni vichwa mitumba na mabehewa mitumba ya mwaka '1947'!.
2. Mkataba ni wa ukarabati na kutiwa nakshi nakshi kwa vichwa na mabehewa mitumba!, na sio kuundwa kwa vichwa na mabehewa mapya!.
3. Hakuna ubaya nchi kununua vichwa mitumba na mabehewa mitumba, kitu muhimu ni Watanzania tuelezwe ukweli!.
4. Je, hivyo vichwa viliundwa lini, wapi na vimetumika muda gani kabla sisi hatujauziwa?
5. Mitumba hiyo imenunuliwa kwa bei gani na inakarabatiwa kwa bei gharama gani?
5. Tufanyiwe comparative analysis, kama tungenunua vichwa vipya na mabehewa mapya, tungetumia gharama kiasi gani, compared na kununua vichwa mitumba na mabehewa mitumba, ili tujue tumeokoa fedha kiasi gani kwa kununua mitumba hiyo?
6. Japo gharama za kununua vitu vipya ni juu ila maintance cost ni ndogo, unaweza kununua mitumba kwa bei poa kumbe ni mitumba choka mbaya, hivyo maintenance cost ikawa juu.
7. Sii wengi wanajua kazi ya CAG sio kutoa tuu zile ripoti za hesabu za serikali, CAG ni Mdhibiti na Mkaguzi, ufhibiti unafanywa kabla ya manunuzi, je, kulifanyika tathmini yoyote rail worthness report ya vichwa mabehewa hayo mitumba kabla hayajanunuliwa?. Then CAG atufanyie value for money audit, msikute mitumba hiyo tumepewa bure, huku watu wakipiga kubwa tunauziwa kwa bei ya mapya!.
8. Ukiingia mkataba wa manunuzi, mzigo ukanunuliwa, delivery ndio ikachelewa, huwezi kuvunja mkataba huo ukabaki salama, hivyo kesi ikifunguliwa, Tanzania tunashindwa hata kabla kesi haijaanza!.
9. Tulivunja mkataba wa Dowans, tulishitakiwa, tukashindwa, tukadaiwa tukasema hatulipi!, watu wakajiapisha "over my dead body", hatulipi!.
ukweli ni kuwa tumelipa kwa siri, Watanzania hatukuambiwa!.
10. Tulipo vunja mkataba wa Dowans, Zitto akashauri tuitaifishe mitambo ile, Wabunge wetu wakagoma kuwa Tanzania hatununui mitambo chakavu, mitambo mitumba!
11. Mitambo ile ikanunuliwa na Simbion, tukaingia nao mkataba ule ule wa Dowans, watu wale wale walio ikataa dowams, ndio hao hao danced to the tune na Hilary Clinton kuzindua Simbion kwa mkataba ule ule tuliovunja!, kwa gharama zile zile!, na capacity charge ile ile!, na tukawalipa!.
12. JPM alipoingia tukavunja mkataba wa Simbion, tukashitakiwa, tukashindwa, JPM akagoma kulipa!, ila baada tuu ya JPM kuitwa kule, huku nyuma, sio tuu tumelipa, bali pia tumeinunua ile mitambo Simbion kwa bei ya ajabu!, sasa mitambo ile tuliosema ni chakavu, mtumba, na serukali yetu hatununui, vitu chakavu, sasa ndio tumeinunua, sasa mitambo ile ni mali yetu! na malipo yote yaliisha fanyika chap chap fasta!, ila Watanzania hatuambiwi!.
Watanzania wa sasa ni waelewa, tuwe tuu tunaambiwa ukweli, tutaelewa tuu kuliko...
Wasalaam.
Paskali.