Hongera TRL kwa Mabehewa Mapya. SGR ni Reli Mpya ya Kisasa; Je, Mabehewa Haya ni Mapya ya Kisasa? Hakuna Ubaya Kutumia Mitumba, Ila Tuambiwe Ukweli!

Narudia kukuuliza umesoma mwanzo wa mada na kujua kinachojadiliwa? Naona kama umeibuka tu
 
Wanajitekenya, na kucheka wenyewe......Taarifa ya awali inaonyesha ni ya mtumba yaliyokuwa yanakarabatiwa.......hapa wameyashusha yakiwa ndani ya makaratasi! Kama bidhaa mpya i.e simu. Inachekesha mnoo.

Utakuta kwenye makabrasha wameandika bei ya mabehewa mapya...ndio maana yamekuja yakiwa ndani ya makaratasi kabisa ILI kuuaminisha umma.
 
My point; Watanzania ni watumiaji wazuri wa vifaa used na hatuoni ubaya wowote kutumia hivyo vitu yaani used au mitumba, Ila kitu muhimu muhimu ni tuambiwe ukweli wote!.
Siadhani kwamba watanzania wanapenda kutumia mitumba hii inatumika kwasababu hakuna jitihada zinazofanyika ili kuweza kutengeneza vya kwetu au naweza kusema uwezo wetu kiuchumi unatulazimisha kununua mitumba.
Pia hii sio sifa nzurii ya kutumia mitumba kwenye miradi mikubwa ya kitaifa haifai kuwa na mitumba,pia sidhani km niwe angekuwepo angeruhusu hii mitumba jamaa alikua ni mtu smart japo alikua na kasoro zake
 
Kwenye mambo ya SGR, Watanzania tunapaswa kuambiwa ukweli wa kila kitu!, serikali yetu lazima iwe very transparent see through kwenye kila kitu including mikataba na financial maters kufuatia kuwahi kupigwa huko nyuma kwenye rada, kwenye ndege, kwenye meli na sasa kwenye reli
Maswali haya yajibiwe kikamilifu
Maswali haya yanahitaji majibu ya kina na sio blah blah!.
Kama mtu kuuliza maswali kama haya, kutapelekea kuhojiwa uzalendo wake, mimi naomba kutumia kinga ya kihabari na kanuni ya kwanza ya mwandishi wa habari no seek the truth, and write nothing but the truth!, kuna kitu ninadhamiria sio tuu kuandika bali kukitengenezea a video documentary ya safari ya SGR ya Tanzania, tulipotoka, tulipo na tunapokwenda, ili huko mbele, likija kujitokeza liji white elephant fulani hivi ambalo sijui kama ni mimi tuu naliona, angalau dhamira yangu isinisute, niliona kabla, nikasema kabla, nikaandaa documentary kabla, nikaonyesha kabla, ili angalau jamii ya Watanzania wajue kuna watu waliona kabla na walisema kabla!.

Na labda kuwasaidia Watanzania wenzangu wasio jua, kwenye ile kashfa ya rada, BAE walikiri kutoa mlungula wa kickbacks, lakini sheria yao inawaruhusu non disclosure ya waliowapa mlungula, ilo usipoteze wateja wapya wapenda mlungula, kibiashara mlungula wa 10% ni halali!, ila ikijulikana kuwa umetoa mlungula, unapaswa ama uwataje uliowapa mlungungula, wakamuliwe wautapike huo mlingula, ama uwahifadhi usiwataje, na badala yake utozwe faini kwa uliowapa mlungula, na kuurejesha ule mlungula, na hicho ndicho kilichofanywa na BAE, kuwahifadhi waliowapa mlungula, na badala yake ikakubali kulipa faini na ndipo tukarejeshewa ile chenji ya rada.

Hii maana yake, kuna viongozi wetu walikula mlungula BAE akawakingia kifua kuwahifadhi kwa kulipia faini na ule mlungula ukarudishwa nchini kama chenji ya rada, endapo BAE wasinge wakingia kifua kuwahifadhi na kuwalinda, amini usiamini, hayo majina ya waliopokea mlungula na kuzihifadhi fedha zao kule Credit Suisse, yangetoka, Watanzania msinge amini macho na masikio yenu!.

Kashfa hii iliobuka kwasababu tuu kulitokea lijinga limoja, mgao wake yeye ukauhifadhi visiwa fulani ambavyo viko chini ya milki ya Uingereza, ndipo Muingereza akabaini, lakini kama wote wange bank Swiss banks, kule fedha zao ni very secure, hata bank manager, hajui majina ya customers na clients ni secret codes tuu zinatembea, hivyo wala kashfa ya rada isinge ibuka!.

Hivyo watu tunaoulizia kuhusu haya mabenewa, naomba mtuelewe ni wazalendo wa kweli wa nchi hii!.

Paskali
 
Tuipongeze serikali kwa kuchukua mitumba ya S. Korea ni wazi imefanyiwa recondition. Kwani kungekuwa na uwezekano wa kuchukua mitumba ya China ama India, si kwamba uwezekano huu umefutika, mbele ya safari huwezi jua lakini angalau mwanzoni ubunifu makini umetumika. Na amini wamekumbuka kuyafanyia fermigation tusije tukazalisha hapa nchini tatizo la mende wa Kikorea.
 
Mitumba ya South Korea mizuri kuliko ya China na India

Hata nguo za mitumba au magari mitumba Tanzania hatuagizi China wala India
 
We nae uzuzu utakuisha lini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…