Hongera uongozi wa Simba kwa website bora

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Nahisi kama nimechelewa kulifahamu hili. Leo asubuhi katika pita pita zangu nimekuta na website bora kabisa, narudia bora kabisa kuwahi kuiona. Kwanini nasema hii website, ni bora sana:

1. Ni website ambayo inajazwa habari za mnyama as soon as it happen. Mfano, sikua nikifafamu kuwa "mtalamu" Nico Kiondo anatutengenezea timu ya vijana kuanzia miaka 15-18 kupitia kitu kinaitwa Simba Vipaji.

2. Sasa hata ukiwa kijiji cha Tanganyika-Magati kilichopo Kata ya Mlimba, Ifakara, katika wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro unaweza kujipatia uanachama wako wa Simba SC kupitia simu yako.

3. Lile suala la kuvaa jezi feki limefikia mwisho. Kuanzia sasa kupitia website yetu "pendwa" tutaweza kununua jezi, traki suti, skafu, boksa, shuka, top kwa ajili ya madada zenye logo ya Simba Sc zitapatikana katika maduka tutakayoelekezwa. Maduka hayo yatasambaa nchi nzima.

4. Kitu kingine kizuri ni kuwa, Kosi zima litakalochukua ubingw msimu ujao lipo ndani.. Pia technical bench wakiongonzwa na Kocha mwenye Leseni ya Grade A toka UEFA "mtalamu" Dylan Kerr nalo ndani.

5. Kuna mapicha mbali mbali ya mashabiki wakishangilia time yao pendwa.. Chakufurahisha ni kuwa hata mimi picha yangu IPO nikishangilia goli la Okwi alilowafunga Mtibwa taifa.. Ama kweli Simba SC ni ya watu wote.

Asante sana Evance Aveva, kwa kumtafuta mtu makini Iman Kajula anayeeongoza kampuni bora kabisa kwa sasa nchini EAGgrop iliyotutengenezea http://simbasports.co.tz/ ambayo ni website bora kabisa kuwahi kutokea Africa Mashariki na Kati a.k.a CECAFA.
I wish kungekua na mashindano ya website bora za vilabu vya soka kama ilivyo uingereza ambapo kila mwaka Arsenala anachukua (ni mtizamo tu, mtani usijenge chuki)

Link yenyewe ni:http://simbasports.co.tz/
 
Nahisi kama nimechelewa kulifahamu hili. Leo asubuhi katika pita pita zangu nimekuta na website bora kabisa, narudia bora kabisa kuwahi kuiona. Kwanini nasema hii website, ni bora sana:

Link yenyewe ni:Simba Sports Club | Simba Sports Club

Safi sana, Mbuyu ulianza kama mchicha pia..

Ila nawashauri tu waangalie hadhira (Audience) yao ni kina nani, wengi wao kizungu sio lugha yao. Na kama hivyo ndivyo basi ni bora waweke kila kitu kwa kiswahili tu.
 
Hiyo website naona wanachelewa sana kutoa taarifa mpya wanashindwa hata viblog vodogo vidogo na magazeti ya ajabu ajabu. Hata wangetuma mwandishi lushoto bado wangepata habari nyingi za kuandika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…