LGE2024 Hongera wanaccm kujitokeza kwa wingi na kuonyesha mfano wa kizalendo katika zoezi la kujiandikisha kwajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

LGE2024 Hongera wanaccm kujitokeza kwa wingi na kuonyesha mfano wa kizalendo katika zoezi la kujiandikisha kwajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Kwa hakika mmeupokea na kuitikia vema wito na wa Rais na Mwenyekiti wa CCM taifa Dr Samia Suluhu Hassan wa kujitokeza kwa wingi, katika zoezi la kujiandikisha kwajili ya uchaguzi wa serika za mitaa katika siku hizi za mwanzo kabisa.

Ama kwa hakika,
biashara ni asubuhi.
Shime waTanzania wote wenye sifa na vigezo vya kupiga kura, tukajianzikishe kwa wingi, ili tupate fursa na haki ya kuchagua viongozi watakao tuongoza, hususani kwenye mazingira tunamo ishi tar 27 Nov. 2024🐒

Mungu Ibariki CCM
Mungu Ibariki Tanzania
 
Huo uchache unaouona ndio uhalisia wa kura za ccm miaka yote, ila wapinzani wakijazana ndio huwa wanapora kura na kujitangaza wao. Safari hii watu wanaojitambua wamegoma kujitokeza, na siku ya uchaguzi ndio utaona idadi ndogo sana ya wapiga kura.
 
Hivi mtu akijiandikisha unajuaje kuwa atampigia kura chama flani?
 
wew sio mwana ccm unababaika nini gentleman 🤣

mie nimewapongeza wana CCM na sio vinginevyo🐒
 
Hivi mtu akijiandikisha unajuaje kuwa atampigia kura chama flani?
kwa wana CCM ni rahisi sana,

wanakusanyana nyumba kwa nyumba, wanakutana kwa pamoja ofisi za CCM zilizo karibu na kituo cha kujiandikisha, wanahamasishana, wanaelekezana na kutambuana wao kwa wao, kwamba nani yupo na nani hayupo, wanaamua, kisha wanaelekea kituoni kujiandikisha au kupiga kura..

CCM huwa ni ndugu wenye umoja na upendo sana, ndio maana wao na ushindi wa kishindo ni dam dam 🐒
 
Back
Top Bottom