Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Sasa ni dhahiri Wananchi wa Tanzania wamekomaa kimawazo na kiakili , nimepita maeneo kadhaa ya jiji la Dar es Salaam , liliwemo eneo korofi la Kariakoo nimeshuhudia hatua kadhaa za kujilinda na maambukizi zikichukuliwa na wananchi wenyewe huku wakihamasishana kujifanyia usafi wa mikono kwa maji tiririka , almost 70% wamevaa barakoa , japo barakoa zingine hazina ule ubora unaostahili.
Nachukua nafasi hii kuwapongeza wananchi kwa kustuka na kuamua wenyewe kujiepusha na matatizo , namuomba Mungu aweke mkono wake wa ulinzi juu ya vichwa vyao.
Hapa chini naambatanisha mchoro unaoelekeza namna nzuri ya kunawa mikono.