Hongera Watanzania kwa kuamua wenyewe kuchukua tahadhari dhidi ya Corona

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Sasa ni dhahiri Wananchi wa Tanzania wamekomaa kimawazo na kiakili , nimepita maeneo kadhaa ya jiji la Dar es Salaam , liliwemo eneo korofi la Kariakoo nimeshuhudia hatua kadhaa za kujilinda na maambukizi zikichukuliwa na wananchi wenyewe huku wakihamasishana kujifanyia usafi wa mikono kwa maji tiririka , almost 70% wamevaa barakoa , japo barakoa zingine hazina ule ubora unaostahili.

Nachukua nafasi hii kuwapongeza wananchi kwa kustuka na kuamua wenyewe kujiepusha na matatizo , namuomba Mungu aweke mkono wake wa ulinzi juu ya vichwa vyao.

Hapa chini naambatanisha mchoro unaoelekeza namna nzuri ya kunawa mikono.

 
Jambo jema kabisa hili.....wabarikiwe wote wenye upeo huu wa hali ya juu kabisa, kwa mustakali wa maisha yetu....
 
Anae sema hakuna CORONA yupo chato kajificha akiwa chini ya uangalizi mzito wa madaktari.
SIASA IACHE KUINGILIA FANI/TAALUMA ZA WATU HASWA ZA ZINAZOGUSA UHAI WA RAIA NCHINI.
 
kila mtu ni kujikinga tu kama unaogopa kufa kama ni shujaa huogopi kufa basi huna haja ya kujivalisha mazonge.
 
Asilimia 70 gani hiyo ya waliovaa barakoa hapa kariakoo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…