Hongera Wizkid Kwa kuchukua Tuzo! Ulistahili!

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Usiku wa jana Tuzo za MTV mama Zilitolewa huko South Africa! Wanigeria waliibuka vinara baada ya kuchukua tuzo nyingi kuliko nchi yoyote Afrika! Na zile tuzo kubwa zote zilienda Nigeri kama Best Male na Best Female pamoja na Artist of the Year!

Hongera wizkid pamoja na Yemi Alade kwa kuchukua Tuzo hizo! Fact ni kuwa sasa Wabongo hatuhitaji kumtafuta mchawi ni nani katika tuzo hizi ila inatakiwa tujifunze na Tufanye mambo makubwa sana mwaka Ujayo!

Ni kawaidaa yetu wabongo kutokubali ukweli ila kiuharisia hizi tuzo watanzania hata tungekuwa wengi kiasi gani walioshiriki hizi tuzo walikuwa katika vipengele vigumu sanaaa tofauti na uwezo wao! Angalia Rayvanny hana mafanikio makubwaa ingekuwa vigumu kushinda mbele ya Tekno aliekuwa vizuri sana Mwaka huu hata wabongo tungekuwa wengi kiasi gani na kwa umoja gani hiyo tuzo ingekuwa vigumu sana kutokana alie shiriki kutokuwa na Mafanikio!

Vipengele ambavyo mimi nilikuwa navitazama ni best male,artist of the year,na best Female! Ila vingine vyote wabongo tuliwekwa ili kunogesha Mashindano...Na vingine tulibebwa na watu hatukustahili kuwepo huo ndo ukweli!

Hizi tuzo mshindi anapatikana kwa njia ya kupigiwa kura ila sidhani kama Kura ndo zinasema mshindi ni nani waandaji wanatakiwa kutwambia kilicho nje ya kura! Kinachonifanya niseme hivi ni hivi Hawa walio kuwa wanawania kipengele cha Best Male in Africa ndio wale wale Walio wania Best MALE IN AFRIKA katika tuzo za BET na wapiga kula ni wale wale na Team zetu ni zile zile na population ni ile ile Iweje mtu anapata tuzo BET halafu anakosa MTV Mama kama kigezo ni kura?

Iweje mtu anakosa tuzo BET anapata MTVMama akati wapiga kura ni wale wale na hamna kipya kilichofanyika? Waandaji wanapaswa kutuambia kilicho nyuma ya Tuzo hizi! Ila kwa kigezo cha Kura huo ni uongo!

Diamond kurudi tena kushiriki hizi tuzo ni jambo kubwa na kumbuka DAVIDO Hajarudi wala Psquare lakini kiuharisia mwaka huu diamond hakufanya vizuri yeye kama yeye maana Katoa wimbo Mmoja katika mwaka kabla ya tuzo ila kashirikishwa sanaaa! Huku wizkid akiwa na Ojuolegba na Final! Kiuharisia Diamond hakuwa na nafasi kubwa ya kushinda mbele ya Wizkid Tukumbuke Skeleu ilimpa tuzo Davido!

Kwa upande wangu nasema Hongera Wizkid ulistahili hii tuzo Ila kura sio kigezo wabongo hata tungelala tunavote! Angalia na mfumo ulio tumika kuvote!! Kikubwa tuongeze juhudi
 
Anastahili kwa kweli... [HASHTAG]#starboy[/HASHTAG]
 
Mwaka huu kura zangu haziku haribika kabisa, hongera wizkid, hongera yemi alade, hongera tekno.
Watanzania wenzangu tujitaidi kutengeneza mziki mzuri, tuachane majungu na maneno maneno.
 
mond hajang'ara mwaka huu nyimbo zina viewer wachache siyo kama zamani
 
Vile Wizkid anaimba kama Msagasumu akiwa kabeba mwali" haya Igaa tena na hii,haya chukua tena na hiii..." wengine wamejitahidi hasa wasanii wetu
 
Yes,Wizkid ANASTAILI na hongera kwa wote waliokuwa nominetedi ndio ushindani ulivyo anatakiwa mmoja ndio ashinde,ni kama inavyokuaga Wizkid anapokosa tena yeye huwa anaenda mbali zaidi kwa kuziponda akikosa,lakini nenda kamuulize leo baada ya kushinda kama ataziponda......Na watu wasifikiri sababu ya kukosa ni UTIMU SI KWELI KWA MAANA WIZKID NI MARA NGAPI ANAKOSA,KWANI NA WAO KWAO KUNA UTIMU ........LAKINI SI MBAYA DIAMOND KAKOSA HUKO KAPATA HUKU,KAMA NI SWALA LA UTIMU HATA HUKU ANGEKOSA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…