Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 390
- 1,425
Jana nimeona mashabiki chawa wote wa Simba waliamua kufunguka dhidi ya uongozi wa timu yetu ambayo wanajifanya kutia pamba masikioni, tulianza kuwaambia viongozi since day walipoanza kufanya usajili kuwa timu yetu haina wachezaji wazuri, wachezaji tuliokuwa nao hawawezi kutufikisha popote, wanatusoma na kisha wanatusonya, wakawa wanatupa matumaini ya kitoto kabisa kuhusu uwezo wa wachezaji wetu lkn hatukukubali, msimu umeanza na ukwel umeanza kubainika, kiukweli viongozi wa Simba mnatukosea sana.
Haya mambo haya kwa wale waliokuwepo miaka ile ya 90, wamuulize Jimmy David Ngonya, walikuwepo akina marehemu Priva Mtema, Juma Salum, wako wapi.Muulizeni Azim Dewji wakati ule Boli Zozo anatudhalilisha pale uwanja wa shamba la bibi, au muulizeni mzee Dalali yaliyowahi kumkuta kwa kuifanyia maudhi Simba.
Miaka ya hivi karibuni tumekuwa wastaarabu sana, mnafanya mnachoweza ndani ya klabu yetu mkijua hakuna la kuwafanya, mnagombana wenyewe kwa wenyewe kila siku kwa kutaka maslahi binafsi na tunaona mkipatanishwa laivu, haya mambo mbona hatuyaoni kule yanga? Hivi kiuhalasia tuachaneni na siasa, ukiangalia mchezaji mmoja wa Simba, ana quality kweli ya wachezaji wa Yanga, hiv Dennis Nkane kwa wachezaji wa Simba wa sasa hivi nani wa kumweka benchi, sure boy, Farid Mussa, Mauya, Makambo, Ambundo hawa Simba hii hawakai benchi, hivi kocha Mgunda afanye maajabu gan kwa wachezaji wale, Kibu Dennis? Kweli, kweli, kweli, Nyoni? Bocco?, Mwinuke? Kyombo?, Banda? Akpan? Okwa? Kanoute anayecheza kiungo ya kizamaani, Mkude? Halafu tujisifie kuwa tuna timu?
Shame on you viongozi wa Simba, timu haieleweki, Barbra kakimbia Morroco kwenye timu ya wanawake.
Mngejua uchungu, ghadhabu, hasira na jakamoyo niliokuwa nalo dhidi yenu, ningekuwa na uwezo ningewameza wote nyie.
Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app