Hongereni mashabiki Chawa wa Simba kwa kuwapa makavu viongozi wetu

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Jana nimeona mashabiki chawa wote wa Simba waliamua kufunguka dhidi ya uongozi wa timu yetu ambayo wanajifanya kutia pamba masikioni, tulianza kuwaambia viongozi since day walipoanza kufanya usajili kuwa timu yetu haina wachezaji wazuri, wachezaji tuliokuwa nao hawawezi kutufikisha popote, wanatusoma na kisha wanatusonya, wakawa wanatupa matumaini ya kitoto kabisa kuhusu uwezo wa wachezaji wetu lkn hatukukubali, msimu umeanza na ukwel umeanza kubainika, kiukweli viongozi wa Simba mnatukosea sana.

Haya mambo haya kwa wale waliokuwepo miaka ile ya 90, wamuulize Jimmy David Ngonya, walikuwepo akina marehemu Priva Mtema, Juma Salum, wako wapi.Muulizeni Azim Dewji wakati ule Boli Zozo anatudhalilisha pale uwanja wa shamba la bibi, au muulizeni mzee Dalali yaliyowahi kumkuta kwa kuifanyia maudhi Simba.

Miaka ya hivi karibuni tumekuwa wastaarabu sana, mnafanya mnachoweza ndani ya klabu yetu mkijua hakuna la kuwafanya, mnagombana wenyewe kwa wenyewe kila siku kwa kutaka maslahi binafsi na tunaona mkipatanishwa laivu, haya mambo mbona hatuyaoni kule yanga? Hivi kiuhalasia tuachaneni na siasa, ukiangalia mchezaji mmoja wa Simba, ana quality kweli ya wachezaji wa Yanga, hiv Dennis Nkane kwa wachezaji wa Simba wa sasa hivi nani wa kumweka benchi, sure boy, Farid Mussa, Mauya, Makambo, Ambundo hawa Simba hii hawakai benchi, hivi kocha Mgunda afanye maajabu gan kwa wachezaji wale, Kibu Dennis? Kweli, kweli, kweli, Nyoni? Bocco?, Mwinuke? Kyombo?, Banda? Akpan? Okwa? Kanoute anayecheza kiungo ya kizamaani, Mkude? Halafu tujisifie kuwa tuna timu?

Shame on you viongozi wa Simba, timu haieleweki, Barbra kakimbia Morroco kwenye timu ya wanawake.

Mngejua uchungu, ghadhabu, hasira na jakamoyo niliokuwa nalo dhidi yenu, ningekuwa na uwezo ningewameza wote nyie.

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
 
Acha zako wewe,hakuna timu ambayo haihitaji maboresho haohao yanga uliowataja wiki iliyopita kabla ya marudiano na africain kila mtu alisema ni timu ya kawaida,leo unaibeza simba kuna timu imefunga magoli mengi kuliko simba mpaka sasa kwenye ligi kuu?kuna timu ipo club bingwa afrika zaidi ya simba?

Hao yanga wameshinda kigoli kimoja dhidi ya kmc kwa mpira mbovu,wakashinda kwa makandokando dhidi ya geita gold hukuona?shabiki mzuri ni yule anaetoa ushauri wa kujenga.Ni kweli timu yetu inahitaji kuwa na kocha wa viungo,timu inahitajika beki no 2,3,inahitaji striker na kiungo no 6.
 
Simba haina shida kubwa kama unavyoelezea hapa, Simba pale tunahitaji sana Striker namba tisa ya ukweli nilidhani Phiri anakaa pale kati ila naona kama kocha huwa anapenda kumuanzisha pembeni. Mwininge ni kiungo mshambuliaji hatari kama Chama.

Maana siku Chama akikosekana unaona kabisa team ina struggle sana kutengeneza clear cut chances, mwisho ni kiungo mkabaji mmoja matata ilikuwa kosa kubwa sana kumuacha Lwanga alikuwa msaada sana hasa game zinazohitaji nguvu na kukaba zaidi. Nafasi nyingine zote ziko covered vizuri, kwenye hiyo list yako Peter Banda mtoe dogo ni mtu na nusu mtamuelewa soon
 

Wale dawa yao kuwasusia kwenda uwanjani. Unashindwa kumsajili manzoki unaleta mzungu asiyeeleweka.
 
Jana nimeona mashabiki chawa wote wa Simba waliamua kufunguka dhidi ya uongozi wa timu yetu ambayo wanajifanya kutia pamba masikioni, tulianza kuwaambia viongozi since day walipoanza kufanya usajili kuwa timu yetu haina wachezaji
Ngoja ndugu zako waje wakutukane na kukuhusisha na timu ya wananchi.
 
Mimi nilishasemaga kwamba
Okwa
Mzungu
Akpan
Bocco
Nyoni
Mwanuke
Kibu

Kwakweli kwa dirisha dogo wasepe tu lakini hapo bado naangali kwa ndani ni nani atapatikana???
 
Kiungo simba haina ulete striker assist apewe na kanoute?
 
Hawa ni mashabiki wa matokeo ni washamba sana aseee.hivi mtu anatarajia timu ishinde kila siku jamani!!!timu gani huwa inafanya hvyo???
1.kmc 2.Azam 3,yanga 4.singida

Izo ndo team ngumu na Simba hajapata matokeo kwaizo team asa apo unasema unq kikosi?
 
Gombaneni tu Ila msing'oe viti taifa
 
Mimi nilishasemaga kwamba
Okwa
Mzungu
Akpan
Bocco
Nyoni
Mwanuke
Kibu

Kwakweli kwa dirisha dogo wasepe tu lakini hapo bado naangali kwa ndani ni nani atapatikana???
Kwani wewe ni nani? Unachangia shs ngapi za usajili? Acha ushabiki maandazi hapa.
 
Mimi nilipenda build up ya goli la simba dhidi ya ihefu nikajua simba inawachezaji wazuri shida hivi vitimu vinaikamia simba sababu ya bahasha
Ulianza vizuri kama shabiki halafu ukamaliza ovyo kama mshangiliaji. Hakuna timu inapewa fedha icheze jihadi dhidi ya Simba. Hizo ni sababu za kuwafichia udhaifu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…