Kwanini unahangaika kumjibu mtu aliyevimbiwa mihogo, Simba hata kama tuna tatizo Huwa hatuhusushi matatizo yetu na utopoloAcha zako wewe,hakuna timu ambayo haihitaji maboresho haohao yanga uliowataja wiki iliyopita kabla ya marudiano na africain kila mtu alisema ni timu ya kawaida,leo unaibeza simba kuna timu imefunga magoli mengi kuliko simba mpaka sasa kwenye ligi kuu?kuna timu ipo club bingwa afrika zaidi ya simba?
Hao yanga wameshinda kigoli kimoja dhidi ya kmc kwa mpira mbovu,wakashinda kwa makandokando dhidi ya geita gold hukuona?shabiki mzuri ni yule anaetoa ushauri wa kujenga.Ni kweli timu yetu inahitaji kuwa na kocha wa viungo,timu inahitajika beki no 2,3,inahitaji striker na kiungo no 6.
Kwani malalamiko yako hasa ni yepi, maana umesema kila kitu mpaka CEO kwenda kuiona Timu yake ya Wasichana hutakiJana nimeona mashabiki chawa wote wa Simba waliamua kufunguka dhidi ya uongozi wa timu yetu ambayo wanajifanya kutia pamba masikioni, tulianza kuwaambia viongozi since day walipoanza kufanya usajili kuwa timu yetu haina wachezaji wazuri, wachezaji tuliokuwa nao hawawezi kutufikisha popote, wanatusoma na kisha wanatusonya, wakawa wanatupa matumaini ya kitoto kabisa kuhusu uwezo wa wachezaji wetu lkn hatukukubali, msimu umeanza na ukwel umeanza kubainika, kiukweli viongozi wa Simba mnatukosea sana.
Haya mambo haya kwa wale waliokuwepo miaka ile ya 90, wamuulize Jimmy David Ngonya, walikuwepo akina marehemu Priva Mtema, Juma Salum, wako wapi.Muulizeni Azim Dewji wakati ule Boli Zozo anatudhalilisha pale uwanja wa shamba la bibi, au muulizeni mzee Dalali yaliyowahi kumkuta kwa kuifanyia maudhi Simba.
Miaka ya hivi karibuni tumekuwa wastaarabu sana, mnafanya mnachoweza ndani ya klabu yetu mkijua hakuna la kuwafanya, mnagombana wenyewe kwa wenyewe kila siku kwa kutaka maslahi binafsi na tunaona mkipatanishwa laivu, haya mambo mbona hatuyaoni kule yanga? Hivi kiuhalasia tuachaneni na siasa, ukiangalia mchezaji mmoja wa Simba, ana quality kweli ya wachezaji wa Yanga, hiv Dennis Nkane kwa wachezaji wa Simba wa sasa hivi nani wa kumweka benchi, sure boy, Farid Mussa, Mauya, Makambo, Ambundo hawa Simba hii hawakai benchi, hivi kocha Mgunda afanye maajabu gan kwa wachezaji wale, Kibu Dennis? Kweli, kweli, kweli, Nyoni? Bocco?, Mwinuke? Kyombo?, Banda? Akpan? Okwa? Kanoute anayecheza kiungo ya kizamaani, Mkude? Halafu tujisifie kuwa tuna timu?
Shame on you viongozi wa Simba, timu haieleweki, Barbra kakimbia Morroco kwenye timu ya wanawake.
Mngejua uchungu, ghadhabu, hasira na jakamoyo niliokuwa nalo dhidi yenu, ningekuwa na uwezo ningewameza wote nyie.
Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
We ndio unajua mpirqSimba haina shida kubwa kama unavyoelezea hapa, Simba pale tunahitaji sana Striker namba tisa ya ukweli nilidhani Phiri anakaa pale kati ila naona kama kocha huwa anapenda kumuanzisha pembeni. Mwininge ni kiungo mshambuliaji hatari kama Chama.
Maana siku Chama akikosekana unaona kabisa team ina struggle sana kutengeneza clear cut chances, mwisho ni kiungo mkabaji mmoja matata ilikuwa kosa kubwa sana kumuacha Lwanga alikuwa msaada sana hasa game zinazohitaji nguvu na kukaba zaidi. Nafasi nyingine zote ziko covered vizuri, kwenye hiyo list yako Peter Banda mtoe dogo ni mtu na nusu mtamuelewa soon
Yanga wanajificha kwenye matatizo ya simba ila kiukweli kwa wanaojua mpira pale hamna team wachezaji wote wazee wale wamebakisha msimu mmoja tu wastaafu ukimtoa yule msheri na nkane pamoja na feisal na yule dogo wa jana wote wazee na yule mwinyi zahera alishasema yanga ikija kukutana na team zenye kasi kama vipers na wale al hilal hakuna beki wala kiungo wa yanga anagusa mpira.Simba haina shida kubwa kama unavyoelezea hapa, Simba pale tunahitaji sana Striker namba tisa ya ukweli nilidhani Phiri anakaa pale kati ila naona kama kocha huwa anapenda kumuanzisha pembeni. Mwininge ni kiungo mshambuliaji hatari kama Chama.
Maana siku Chama akikosekana unaona kabisa team ina struggle sana kutengeneza clear cut chances, mwisho ni kiungo mkabaji mmoja matata ilikuwa kosa kubwa sana kumuacha Lwanga alikuwa msaada sana hasa game zinazohitaji nguvu na kukaba zaidi. Nafasi nyingine zote ziko covered vizuri, kwenye hiyo list yako Peter Banda mtoe dogo ni mtu na nusu mtamuelewa soon