Hongereni Mashabiki Wa Yanga kwa Ukomavu

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Jana umepigwa mtanange wa watani wa jadi Yanga na Simba na matokeo yake ni Yanga kupoteza kwa mikwaju ya Penati baada ya dk 90 timu zote kutoshana nguvu kwa matokeo ya bila kufungana.

Asilimia kubwa ya Watu walikua wakijua simba atapata ushindi wa kirahisi kutokana na aina ya usajili alioufanya lakini la hasha haikua hivyo Yanga walipambana Wakiongozwa na kiungo fundi/mdukuaji/ Papii Tshishimbi ambaye hajakaaa na timu hata mwezi ila alicheza mpira mzuri mnoo

Licha ya kupoteza kwa Mikwaju ya penati Mashabiki Wa Yanga wamekua watulivu wakijua nini maana ya matokeo ya mpira ila narudia tena ila ingekua ni upande wa pili umefungwa sidhani kama kocha angekua salama mpaka sasa.

Nlichoona Mechi ya jana angalau timu zimeonesha Ufundi na kuacha kucheza kwa kukamiana hongereni kwa hilo.

Tunategemea Michezo mizuri zaidi ijayo na maandalizi mema kwa kuanza msimu wa Ligi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sure akitulia atafika mbali, anacheza mpira mzuri, pia anatumia zaidi akili maana bila yeye niliona goli mbil za wazi.....

Ila Tshimbimbi pale tumelamba dume........! Anajua kuchafua!

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee bila kupepesa macho Hii mutu Ya kongo inajua,Yaa Gadiel alifanya Clearance mbili za wazi kabisa baada ya beki za kati kupoteana,kwa kifupi wajana walijitaidi kutegemea tulikua hatupewi nafasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reactions: Oxx
Jamaa zetu eti wamwetumia 1.5 billion kusajili. Uongo mwingine noma sana. Nadhani wajanja wametengeneza madeni hewa ili mtu apewe timu kiubwete.
 
Sawa ila bila Gadiel kucheza jihad,mpira ungeishia ndani ya dakika 90. Simba pale mbele kuna watu hawaoni goli kabisa.
 
Yanga kwa kweli walifungwa kabla ya mechi naona magazeti yaliwaogopesha maana ata uwanjani walikuja wachache afu walikua na uzuni ata vibandani walikua wachache afu walikua na uzuni kama waliokua uwanjani maana wengi walijua tnafungwa 5 na walipoona wamefika kipindi cha pili awajafungwa walianza shangilia vitu vya ajabu mara tshishimb

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mengi umeyaongea vizuri lakini hukufanikiwa kabisa kuficha mahaba yako kwa vyura fc.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba wanatumia nguvu nyingi kusaka ubingwa...wakatathimini nguvu ya Yanga iko kwa Manji wakambambika mikesi ya ajabu....Yanga akawa bingwa...wakaka chini kubuni mbinu mpya..wakaenda Azam kusomba key players wanne sijawahi kuona duniani kote timu kuuza wachezaji nyota wanne kwa mpinzani..wakarudi mtibwa wakakomba wachezaji lukuki..kama haitoshi wakazoa Niyo na Ngoma akaponyoka...Najiuliza Yanga ni imara sana paka timu tatu kujiunga pamoja kushindana na Yanga..kuna kundi la Simba..Mtibwa na Azam..ciao
 
NNimefarijika saana kwa jinsi timu yangu ilivyocheza.
Nikifikiria bado ninazo hazina za ukweli nje.
1-Chirwa
2-Tambwe
3-Mwashiuya
Ukizingatia ndo mechi yetu ya pili ngumu toka tufanye usajili baada ya mechi na Singida United.

Licha ya kuopoteza wachezaji 3 muhimu bado timu Niko imara saana. Wachezaji tuliopoteza
1-Bossou
2-Haruna
3-Msuva
Hongereni saana viongozi isimamieni timu naona ubingwa wa 4 mfululizo, tulieni tafuteni mchezaji wa kigeni wa ukweli nafasi iliyobaki ikiwezekana mshirikisheni Tshitshimbi kupoint MTU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…