Hongereni sana shule ya Kemebos Secondary School Kagera

big dreamer

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
399
Reaction score
1,076
Mimi kama mdau wa elimu, nimependezwa na kufurahishwa na haya matokeo ya juu kabisa na ya ajabu iliyopata shule hii.

Walikuwa na wanafunzi 70

Wanafunzi wote 70 wamepata div. One

Kupata one pekee sio ajabu sana kwenye nchi maana hata st. Fransis girls Mbeya wanapata n.k n.k, Bethel Mafinga wanapata ila hawa wote wamepata div. One za single digit yani wameishia div ya point 9 tu.

Division one ya point 7 (ambao ndio ufauli mkubwa zaidi ya wote kwa maana waliopata A zote) wapo 62

Div. 1 ya point 8 wapo 5

Div 1 ya point 9 wapo wa 3

Hivyo hakuna aliepata matokeo ya point 10 na kuendelea, aisee hawa jamaa sijui wanatumia mbinu gani za kufundishia hongereni sana walimu na kongole mmliki wa shule za kemebos, mmeupiga mwingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi kama mdau wa elimu,,,nimependezwa na kufurahishwa na haya matokeo ya juu kabisa na ya ajabu iliyopata shule hii


Sent using Jamii Forums mobile app
Wanachagua watoto wenye uwezo mkubwa kuingia nao kidato cha nne.

Lakini bila struggle ya mwanafunzi hakuna kufikia hayo mafanikio. Hivyo tuipongeze shule na wanafunzi
 
Hawa ndio wababe wa St Francis
 
Watakuja watu waseme wamenunua mtihani
 
Mwaka huu wamepitwa na St Francis

Kemebos- GPA ya 1.1024

St Francis- GPA ya 1.0799

GPA inapokua ndogo inamaanisha ufaulu mkubwa
 
Mwaka huu wamepitwa na St Francis

Kemebos- GPA ya 1.1024

St Francis- GPA ya 1.0799

GPA inapokua ndogo inamaanisha ufaulu mkubwa
Labda kwasababu ya idadi ya wanafunzi coz st. Fransis ilikuwa na wanafunzi 90 lakini kemebos wanafunzi 70

St Francis inapoint 10,11 lakini kemebos wameishia point 9 tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera zao...

Huwa nafurahi sana kuona watoto wanapasua pepa kwa wingi...
 
Kuna wale walioonuesha dalili za dv 2,3 walitupiwa shule ya jirani
 
Hiv vipaji huwa vinapotelea wapi lakin ..?
Nipo kukazia tu!
Huku mtaani hatuna umeme, maji, barabara mbovu kichizi, siasa chafi, darasa la saba ni mbunge, n.k n.k; miaka nenda Rudi tuna rundo la wahitimu wenye ufaulu wa daraja la kwanza kwa ngazi zote za elimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…