Horongo juu zaidi ya Usongwe

nyabulo

Member
Joined
Nov 5, 2014
Posts
12
Reaction score
1
Ni shule mbili za sekondari za kata zilizopo bonde la Utengule USONGWE.

Hapo awali zilionekana kuleta upinzani mkali wa ufahulu huku walimu wa shule hizo (Horongo&USONGWE) wakionesha kutambiana kwa kila mmoja kuvutia kwake yeye ni bora ktk ufahulu.

Siku chache zilizopita mwishoni mwa mwaka jana karibu vidato viwili (2&3) vilifanya MOCK na matokeo kutoka mapema mwaka huu na kuonesha HORONGO kuiacha mbali USONGWE kitu kilichopeleka hali ya sintofahamu kwa walimu kutoka USONGWE sekondari wakijiuliza kwanini wamezidiwa na HORONGO sekondari iliyoko kijini zaidi yao.

Wanafunzi wa USONGWE wanapata fursa za masomo ya ziada wakati wenzao wa HORONGO hawana fursa za masomo ya ziada kama za kwao. Nini tatizo apo?
 
USONGWE ni shule ya kata? ivi shule za kata ni zipi kwasababu usongwe ilianza miaka mingi kabla ya hizo shule za kata, pia wana kidato cha tano na sita ambao bila shaka wanatoka sehemu mbali mbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…