HaMachiach
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 3,417
- 6,149
Habali ya jumapili wanabodi,
Napenda kutoa hii taarifa kuhusu hospital ya private ya CHAULA iko Songwe Vwawa. Ukimpelekea mgonjwa wanawapa majibu ya uongo tena magonjwa makubwa ili mtishike haswaa na kuanza kumpa huduma wapate pesa.
Kuna mwanamke alikuwa mjamzito alipoenda pale kupima ultrasound akaambiwa mtoto amekaa vibaya ametanguliza miguu badala ya kichwa hivyo wanaweza mpoteza mama na mtoto kumbe ni uongo, pia kuna mgonjwa alienda kupima pale akaambiwa Figo zimefeli kumbe hakuna kitu.
Kubwa kuliko ni wiki hii tumempeleka mgonjwa wetu pale wakampima x ray majibu wakasema mgonjwa wetu ana saratani kwenye mapafu wakaanza kumtibu na mitungi ya gesi juu tunalipia baada ya kumhamisha hapo tukampeleka hospital nyingine alivyopimwa kumbe anamaji kwenye mapafu, sasa hivi amepewa dawa za kupunguza maji anaendelea vizuri kabisa.
Nitoe rai kwa viongozi wa Mkoa hii hospitali muitazame sana ni waongo mno madaktari wa pale.