Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
SERIKALI imesema Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), itaanza kupandikiza chembechembe hai kwa wagonjwa wa saratani ya damu kuanzia Machi mwaka huu.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, alitangaza neema hiyo jana alipozuru katika hospitali hiyo jijini Dar es Salaam kuona hali ya utoaji wa huduma na vikwazo vinavyowakabili watendaji wake.
Alisema kuna wagonjwa wa saratani ya damu ambao wamekuwa wakisumbuka na kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu hayo, sasa watatibia nchini.
“Wameahidi kunipa andiko zima la namna walivyojipanga na tayari kuna maeneo ambayo wameshaanza kuyafanyia kazi; upandikizaji wa uroto wa mifupa na kumekuwa na wagonjwa wa saratani ya damu, inasuambua watu inabidi wapelekwe nje ya nchi wakafanyiwe vipandikizi vya chembechembe hai.