DOKEZO Hospitali Mpya ya Wilaya ya Butiama ni zaidi ya Miaka Mitano, haijaisha, Watumishi Halmashauri, wanashindana kula PESA

DOKEZO Hospitali Mpya ya Wilaya ya Butiama ni zaidi ya Miaka Mitano, haijaisha, Watumishi Halmashauri, wanashindana kula PESA

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mama Samia , Katika halmashauri iliyojaa wizi ni hii, bahati mbaya sana janja janja hutengenezwa na kupewa Hati safi.

Nendeni mjionee ni nyumbani Kwa Mwl Nyerere lakini majizi hayana Aibu .

Toka Mzee Magufuli alipoanzisha Ujenzi wa Hospitali hizi za Wilaya Tanzania nzima , Katika Wilaya zote nilizopita Hospitali zote zimekamilika Nchini , isipokua Hospitali ya hapo Butiama , majengo pekee yaliyokamilika ni EMD Maternity Complex na OPD peke.

Tena yamekamilika bila vifaa Vyovyote Ndani yake .

Hamna Jengo la Dawa, hamna Maabara, Hamna Mawodi yoyote ya kulaza wagonjwa .

Hamna miundombinu yoyote inayosupport Utoaji wa Huduma, yaan hamna Umeme, Hamna Maji wala hamna mpango wowote wa uvunaji na uhifadhi wa maji hamna Kila kitu .

Halmashauri imeshindwa hata kutengeneza Barabara ya Lami inayotoka Butiama Senta kuelekea Butiama Hospitali.

Ujanja waliotumia kukuficha, ni wamelazamisha kuanzisha huduma za Mama na Mtoto ( RCH) ionekane inafanya Kazi lakini ukweli ni kua Haifanyi kazi.

Kwa Taarifa nilizopewa kutoka Kwa wenyeji na Wafanyakazi wakongwe wa Hospitali ya zamani ya Wilaya Butiama , wanakiri kua

Rais Ulifanya sahihi kumuondoa DED Aliyekuwepo mwanamama Fulani , bahati mbaya hata Huyu DED aliyepo Sasa kaamua kupitia mule mule, Hospital Mpya unatembea mwendo wa kinyonga.

DMOs waliopita katika kipindi hiko chote cha tangu kuanzishwa Kwa Ujenzi wa Hospitali hiyo ya Wilaya hamna lolote wamelifanya.

TAMISEMI wamepeleka DMO mpya ,ambaye ana miezi Kadhaa , angalau katika ma DMOs , huyu anaonekana kua na Msukumo ,Uthubutu na Uwajibikaji hata kusukuma Ujenzi wa Masalia Kwa Kasi kubwa lakini naye changamoto inayompata ni kukoswa uungaji mkono kutoka kwenye halmashauri .

Rais Samia, Waziri Mkuu , Mchengerwa, Muhagama nendeni Butiama, mfike Hospitali Mpya ya Wilaya ya Butiama, msikubali kuhadaliwa na Watumishi wa Halmashauri, mtalia na kutoa machozi.
 
Butiama yetu inashida ya kiuongozi,mfano kuna MKurugenzi yule alikuwa mtoto wa Gaidensia Kabaka yani hajawai hata kuwa mtumishi wala kuwa na cheo chochote Serikalini.
 
Back
Top Bottom