Torra Siabba
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 243
- 287
Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo Jijini Mwanza ni moja ya Hospitali tegemezi zaidi kwa ukanda huu wa Ziwa na hata kwa mataifa ya Afrika Mashariki kutokana na namna walivyojipambanua kuwa wabobezi katika matibabu mazuri kwa binadamu.
Ni jambo ambalo wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa hasa ndio ambao wamekuwa kimbilio katika hospitali hiyo ambayo imekuwa ikiokoa maisha ya waliowengi kutokana na kuwa na vifaa vya matibabu vya kisasa tofauti na Hospitali nyingine pamoja na wataalamu wengi wenye uwezo wa juu.
Wakati Marehemu John Pombe Magufuli alipokua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, manesi na wauguzi katika hospitali hiyo walikuwa wakihudumia wagonjwa vizuri kiasi kwamba watu walivutika na huduma na halikuw ajambo geni kuona wanasifiwa kuwa watumishi wa mfano kwa namna wanavyotibu na kusaidia wagonjwa katika hospitali hiyo.
Kwa sasa wameibuka baadhi ya manesi katika hospitali hiyo ambao wamekuwa wafanyabiashara wakubwa wa nguo za Watoto hususani kwa wale Wanawake ambao ni wajawazito.
Kufanya biashara kujiongezea kipato si jambo baya hata kama unakuwa na ajira nyingine, lakini inatakiwa isiwe kikwazo kwa wengine au isiwe kikwazo kwa wewe unayefanya biashara kushindwa kutimiza majukumu yako ya msingi hasa husuma kwa watu.
Baadhi ya maneso wa hospitali hiyo wanauza bidhaa zao kwa bei kubwa kwa wanawake wanaotarajiwa kujifungua na inapotokea mteja amekataa kununua, basi kanaibuka katabia ka kutomjali mgonjwa hata kama ana tatizo linalohitaji usaidizi, anaweza kufa bila kupewa huduma stahiki kwa kuwa tu wahusika wanajali biashara tu.
Hawa manesi wenye tabia hiyo wamekuwa tishio kwa usalama wa Mama na Mtoto wanaojifungua katika hospitali hiyo, inakera kuona nesi na taaluma yake amekazana kuuza nguo za watoto bila kujali ajira yake ni kusaidia afya za watu kuimarika.
Kwa waliofika levo ya kuwa wazazi au kama wao ni wazazi basi wataelewa kuwa kina mama wote wanaoingia Leba kujifungua wanakuwa nusu kufa au nusu kuishi, sasa badala ya kusaidiwa, manesi wako bize na kufanya biashara, kiukwel inakera sana.
Hivi karibuni kuna nesi mmoja mkongwe alikuwa mkali na kuwapiga mkwara wale manesi wengine ambao wamekuwa na tabia hiyo ya kujali biashara zaidi kuliko majukumu yao ya kazi, lakini inavyoonekana akiwa hayupo, wanaendekea kufanya hivyo kama kawaida.
Pia soma: DOKEZO - Yadaiwa kuwa sababu za vifo vya Mama na Mtoto kuongezeka Hospitali ya Bugando ni mgomo 'baridi' wa Madaktari Bingwa
=================
Updates...
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Thomas Rutachunzibwa alipoulizwa kuhusu madai hayo alisema hana hizo taarifa lakini atafuatilia, baadaye alipotafutwa akasema atafutwe Mkurugenzi wa Bugando ndiye anaweza kutoa ufafanuzi wa suala hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Dkt Fabian Massaga alipoulizwa kuhusu hoja za Mdau akasema “Onana na PRO atakupa ufafanuzi wa kutosha.”
Upande wa Afisa Uhusiano wa Umma wa Hospitali ya Bugando, Evelyne Mahalu amesema “Tunalifanyia kazi kujua ukweli wake, pia BMC ni Taasisi inayosimamia taratibu na miongozo ya Nchi katika suala zima la kuzuia vifo vya mama na mtoto.”