Copro mtego
JF-Expert Member
- Aug 22, 2022
- 619
- 796
Jana nilikuwa nafanya mawasiliano na rafiki yangu aliyempeleka mama yake hospitali ya MKOA MOROGORO.
Aliyoniambia nilishangaa na kusikitisha sana
Kwanza mama alikuwa anaumwa tumbo ameharisha kweli alipewa drip (rl) lakini mtoto wa mgonjwa alilazimishwa kuinunua ilihali mgonjwa ana bima.
Mtoto huyo wa mgonjwa aliambiwa pia alipie dawa ambazo ni drip za metronidazole pamoja na Cipro ndipo alipoanza kufuatilia na kugundua anaibiwa pesa maana bima unalipia hizo dawa
Lakini pia mgonjwa hakufanyiwa kipimo chochote (kwa maelezo ya ndugu wa mgonjwa) vile vile hawakuambiwa nn shida ya mgonjwa na kwa nn amepewa hayo matibabu Kisha mgonjwa aliruhisiwa hivyo hivyo. Hiyo ni kinyume na maadili ya utoaji wa huduma za afya.
Juzi humu JamiiForums tuliambiwa mwanafunzi wa sua alikaa siku mbili bila kupewa huduma inavyotakiwa hadi akapoteza maisha
Tabia hii ya watu wachache inaondoa Imani ya watanzania kwa watoa huduma napendekeza uchunguzi ufanyike ili hospitali itoe huduma kama inavyotakiwa
Haya yalikuwa mawasiliano baina yangu na ndugu wa mgonjwa kwenye picha