Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mkurugenzi mtendaji wa MOI, Prof. Abel Makubi leo amefanya kikao na watoa huduma kwa wateja pamoja na walinzi ili kukumbushana misingi bora ya utoaji huduma kwa wateja na kupunguza mahangaiko na malalamiko kwa wateja.
Kikao hiki ni mwendelezo wa vikao baina ya Prof. Makubi na Makundi mbalimbali ya watumishi wa MOI lengo likiwa ni kutatua changamoto ili kuleta mabadiliko na matokeo chanya katika utoaji huduma kwa wateja.
Mkurugenzi mtendaji wa MOI, Prof. Abel Makubi
Prof. Makubi ameelekeza Menejement yake kuanza utaratibu wa kuwapigia simu au kuwatumia ujumbe wagonjwa wake ili kuwajulia hali, kupata maoni yao na kuwapa ushauri . Utaratibu huu utawezesha wagonjwa kuwa na nafasi ya kutoa maoni au kueleza changamoto zao wakiwa nyumbani kabla ya kurudi tena kliniki za ufuatiliaji.
“Kupitia kikao hiki ni vyema kukumbushana namna sahihi ya upokeaji wa wagonjwa ikiwemo utoaji wa lugha za staha na za kiungwana ili kumfanya mgonjwa afurahie huduma pindi afikapo katika Taasisi yetu ya MOI. Maneno kama karibu sana, pole sanazianze kutawala ndani ya midomo yetu” alisema Prof. Makubi.
Aidha, team za watalaamu na wahudumu zimeelekezwa kuhakikisha zinatoa huduma ya kumuwahi mgonjwa kabla hajatafuta huduma “Rapid response” kwa wagonjwa wa dharura na wale wa kawaida.
“Katika kipindi cha muda mfupi tunatarajia kuwa na eneo mbadala la ndugu wasubiriao wagonjwa kitengo cha dharura (EMD) kwani siyo salama kwa ndugu kubaki eneo hilo wakati huduma za dharura zikiendelea amesema Prof. Makubi.
Akihitimisha kikao hicho Prof.Makubi amewaomba , walinzi, watumishi wa kitengo cha Mawasiliano na kitengo cha uboreshaji wa huduma kuwa na mawasiliano ya karibu sana miongoni mwao na pia kubadilika katika “mindset” na uwajibikaji wa matokeo .