Kabla ya kuanza kulalamikia hospitali husika labda tuanzie na kwa hao watunga sera, wafuatiliaji na mwisho tuchore mstari kuconclude mwananyamala ni machinjio.
Sera yetu inasema huduma kwa mama na mtoto ni bure. Sawa lakini je bajeti inatengwa ya kuziwezesha hospitali kutoa huduma bure?Je inatengwa bajeti ya kuongeza vitanda,majengo?
Ukienda pale mwananyamala kumpeleka mjamzito cha kwanza atapokelewa na maswali lukuki, una pamba,una wembe,una hiki??? utasema ninavyo kitachofuata ni kulala watatu kitanda 1, na kadiri uwingi wa wagonjwa unavyozidi wauguzi wanazidiwa, ratio ya muuguzi kwa mgonjwa inazidi kuwa juu,sasa hapa tena tunarudi kwenye wizara (hawasomeshi wauguzi wa kutosha kukabiliana na wingi wa wagonjwa)
kwa mazingira ya kawaida kabisa mazingira kama haya yanamtia muuguzi huyu katika kuweka vipaumbele wa yupi ahudumiwe mapema. Kama ana ndugu basi ni huyo na akitokea mtu mwenye chochote basi atamhudumia huyo.Haya ni mazingira yanayopelea rushwa japo maadili ya utumishi hayaruhu hata kidogo lakini sera za afyana utekelezaji haviendani.
Serikali inajua kabisa kupitia wizara yake kuwa kina mama wanakufa kama kuku,vichanga ndio usiseme, sasa wao ndio walipaswa kuwa wa kwanza kusimamia sera zake kwa kuweka vipaumbele kwenye bajeti, kuongeza wauguzi(kudhamini elimu kwa waopenda fani ya uuguzi),kuongeza vitanda,wodi za wazazi n.k. Kama mazingira yatawekwa sawa basi naharufu za rushwa zitaanza kupungua.
Niliwahi kumpeleka mama mjamzito pale muhimbili mwaka jana mwishoni, kwa kuwa mazingira ya pale yameboreshwa (majengo yametengenezwa,vitanda kuongezwa na wauguzi,pia idadi ya wazazi imengua kwa kuwa kila mjamzito atastahili kujifungua kwenye wilaya yake husika unless ana referal) mgonjwa wangu alihudumiw kama yupo private, hakukuwa hata kutoa senti.
Tukiangalia kwa macho ya ndani kabisa tutaona kiini hakianzii hospitalini bali huko juu, hela za wizara zinaishia kwenye semina za kujadili kila siku kina mama waboreshere huduma,kwenye semina ndio wanalipana per diem,night allowance na marupurupu kibao at the end of the day hakuna pesa inayoelekezwa panapostahili.Laiti viongozi au watoto wao wangekuwa wanatibiwa mwananyamala,temeke basi leo tungekuw mbali.hata wakiena muhimbili basi wanaenda private(first)track,hapo kweli utamwambia mwananyamala hamna huduma ataelewa?
Serikali: Tekelezeni sera zenu si semina kila siku we want things going not people sitting at discussio rooms for hours.
Mwisho wito kwa wauguzi wetu, japo mazingira ni hafifu msijidhalilishe utu kwa kudai kitu.Thamimini wito wenu uliojaa baraka tele kama mtautekeleza kwa dhati.