Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai Hospitali ya Rufaa ya Iringa inalipisha Huduma ya Vyoo, Afisa Habari wa Taasisi hiyo, Zainab Mlimbila amesema wana Huduma ya Vyoo kwa ajili ya Wagonjwa waliolazwa na vipo vya Wagonjwa wa Nje na watu wengine na kuwa vyote ni bure.
Kusoma hoja ya Mdau bofya hapa ~ Hospitali ya Serikali kwanini inakuwa na huduma ya choo ya kulipia?
UFAFANUZI WA HOSPITALI
Afisa Habari wa Hospitali ya Rufaa ya Iringa, Zainab Mlimbila anaeelezea:
Hospitali yetu ina Vyoo Nane kwa jumla katika majengo tofauti ya Hospitali, kuna Vyoo vya ndani na vingine vya nje, vya Ndani ni vile ambavyo vinatumiwa na Wagonjwa waliolazwa na vile vya nje vinatumiwa na wagonjwa wa nje pamoja na Watu wengine.
Vyoo ambavyo vinazungumziwa vipo kwenye Jengo la Hospitali ambalo limekodishwa kwa mtu, mhusika ameboresha na kuweka vyoo na mabafu ya kulipia.
Vyoo vilivyopo Hospitali sio vya kuoga, vile vya nje katika hilo jengo vinavyozungumziwa vimeboreshwa na vinaruhusu mtu kuoga, hivyo vinatumiwa na watu tofauti wakiwemo wapiti njia.
Jengo hilo lililokodishwa ni la muda mrefu siyo jipya, lipo mpakani na Magereza, mara nyingi ndugu wanaofika kuwatembelea jamaa zao wamekuwa wakifika hapo kuoga na huduma nyingine.
Hospitali yetu ni ya Serikali na haiwezi kuweka vyoo vya kulipia kwa Wagonjwa.