Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Baada ya Wanachama wa JamiiForums.com kuandika hoja zinazoitaja Hospitali ya Muhimbili - Mlonganzila kuwa na gharama kubwa na changamoto nyingine za kiutendaji, taasisi hiyo imetoa ufafanuzi. Kusoka hoja za Wadau bofya hapa chini:
~ DOKEZO: Serikali iimulike hospitali ya Mloganzila, Huduma zake ni janga kwa wagonjwa na ndugu wanaouguza pale
~ Gharama za Kujifungua Hospital ta Taifa Muhimbili MNH (Mloganzila) ni kufuru
UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA ILIYOCHAPISHWA NA MTANDAO WA JAMIIFORUMS KUHUSU HUDUMA ZA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI-MLOGANZILA
DAR ES SALAAM: NOVEMBA 22, 2024
Mtandao wa JamiiForums umechapisha taarifa yenye kichwa cha habari "Serikali limulike Hospitali ya Mloganzila, huduma zake ni janga kwa wagonjwa na ndugu wanaouguza." Kutokana na taarifa hiyo, Uongozi wa Hospitali unapenda kutoa ufafanuzi ufuatao;
1. Wagonjwa 20 hadi 25 kufariki kwa siku
Miaka ya hivi karibuni hadi Novemba 21, 2024, idadi ya wagonjwa wanaoonwa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeongozeka kutoka wagonjwa wa nje 400 hadi 1,000 kwa siku na idadi ya wagonjwa waliolazwa wodini wakati wote imeongezeka kutoka 200 hadi 400 kwa siku. Hii ni kutokana na uboreshaji mkubwa wa mifumo na huduma uliofanywa hospitalini hapo na hatimaye kuvutia wananchi wengi kuitumia hospitali hiyo.
Idadi ya wagonjwa wanaofariki kwa siku hospitalini hapo kutokana na sababu mbalimbali ni kati ya wanne (4) hadi sita (6) kati ya wagonjwa 400 waliolazwa na siyo 20 hadi 25 kwa siku kama ilivyoelezwa katika taarifa iliyochapishwa na JamiiForums.
2. Kutoa taarifa za mgonjwa
Ni kinyume na maadili ya kitabibu kwa mtoa huduma kutoa taarifa za mgonjwa bila ridhaa yake na kwa wale ambao hawajiwezi taarifa hutolewa kwa ndugu aliyeandikishwa au kupewa idhini ya kupokea taarifa hizo (next of kin). Ndugu wengine wanaopenda kufahamu taarifa za mgonjwa wanazipata kutoka kwa mgonjwa mwenyewe au ndugu aliyeandikishwa endapo watapenda kufanya hivyo. Tutaendelea kusimamia jambo hili.
3. Gharama za matibabu kuwa juu
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila inapokea na kuhudumia makundi manne ya wagojwa ambayo ni wagonjwa wa bima, wanaolipa fedha taslimu, wagonjwa wa rufaa wanaochangia huduma na wagonjwa wa msamaha. Mwaka wa fedha 2023/2024, Hospitali imetoa huduma kwa njia ya msamaha zenye thamani ya TZS. 3.9 Bil na kwa robo mwaka wa fedha 2024/2025 huduma zenye thamani ya TZS. 970 Mil zimetolewa kwa wananchi wasiokuwa na uwezo.
Ikumbukwe kuwa, Hospitali hii ni ngazi ya nne (ngazi ya juu) ya utoaji huduma nchini, hivyo teknolojia ya huduma za uchunguzi na matibabu imebalidika kutoka za kawaida kwenda kwenye ngazi za ubingwa bobezi ili kumpa mgonjwa matibabu stahiki. Endapo kuna mgonjwa ana changamoto ya malipo utaratibu wa hospitali uko wazi kupitia Huduma za Ustawi wa Jamii.
4. Kauli za Watoa Huduma
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeendelea kutekeleza azma ya Serikali ya utoaji huduma bora kwa wananchi. Kauli zisizo na staha kutoka kwa watoa huduma zimepungua kwa kiasi kikubwa. Uongozi wa Hospitali hauvimilii kauli za namna hii. Tumelipokea jambo hili, tutaendelea kulifanyia kazi,
Aminiel Buberwa Aligaesha
MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMΜΑ