Hospitali ya Vichaa

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2007
Posts
7,036
Reaction score
9,331
kuna hospitali moja maarufu ya vichaa hapo ndani ya Bongo.
Basi baada ya madaktari kuwa wamefanya kazi nzito na ya muda mrefu ya kuwatibu wagonjwa wao wakaamua wawape test kidogo tu ili wajue wagonjwa wana maendeleo gani.

Basi daktari akawakusanya kwenye wodi kisha akawaambia walie kama kuku.
wengine wakalia "kokolikooo". wengine wakalia "moooooo" wengine wakalia "meeee".wakati huo daktari yeye anachukua data za wagonjwa wake kama kawa.

Basi kuna kichaa mmoja yeye alikuwa kimyaa ameuchuna tu. Daktari akahisi labda huyu atakuwa amepona.akamfuata kumuuliza kwa nini halii kama kuku. basi yule Kichaa akamgeukia daktari kisha akamwambia huku kidole amekiweka mdomoni SHIIII!!!! Nataga!
 
heheee, kweli wee gamba la nyoka ! haya bana angusha nyingine !
 
Hapo ndani bongo we uko kwa yule jamaa Jammeh nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…