Tunaomba TAKUKURU ichunguze mapato ya Hospitali ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi haina Mhasibu yoyote tangu ianzishwe na Mapato ya Hospitali yanakusanywa Jengo la Nje la Wagonjwa (OPD) na Wauguzi ambao sio taaluma yao katika ukusanyaji wa pesa ya Hospitali.
Pia imeonekana na kusadikika kuwa pesa zinatunzwa na Mtumishi fulani wa OPD na kuna wakati watumish katika Hospitali hiyo walitoa mawazo yao kuwa aondolewe haraka huyo Muuguzi anayehifadhi pesa za hospitali lakini Mganga Mfawidhi anamkingia kifua.
Ujumbe huu ufike kwa mamlaka za juu kwa kuwa lengo letu ni Hospitali iweze kunufaika na mapato kwa kuletwa Mhasibu mwenye taaluma hiyo ili kila mgongwa alipe pesa katika njia sahihi.
Kukosekana kwa Mhasibu kunaweza kuwa chanzo cha upigaji na Serikali kupoteza mapato kwa wingi, lakini pia tutambue hii hospitali bado ni mpya inahitaji kuingiza fedha ili huduma ziendelee kuboreshwa.
Majibu ya Hoja soma hapa ~ Katavi: Mganga Mkuu wa Wilaya asema wapo kwenye mchakato wa kuajiri Mhasibu wa Hospitali ya Wilaya ya Mlele