Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwakweli mnachokifanya sio sawa, mnaingilia faragha zetu kwa kutuwekea CCTV camera kwenye vyoo vya kiume vya 'public' vilivyopo kwenye jengo la wodi ya wagonjwa wa nje (OPD) ambavyo vinatumiwa na watu wengi hususani kwenye wodi zilizopo karibu.
Nawaza hata kama mtakuwa hamna nia hasi kwa kusudio la kuweka camera lakini sio katika mazingira ya vyoo ambapo watu ujiachia kufanya mambo yao, kama ni kiusalama tunaweza kubuni njia tofauti na hiyo.
Nikawaza ikitokea kwenye wanaosimamia camera mmoja wao akaamua kuvujisha video za faragha za watu wanaoingia kwenye hivyo vyoo mtakuja kutuambia nini!, tufanye yote lakini tulinde faragha za watu aisee.
Kuna mdau aliandika hapa wengi tukachangia kwa utani lakini ni jambo ambalo lina ukweli 100% mimi nilikuwa pale nimempeleka mdogo wangu kupatiwa matibabu nikaenda kwenye vyoo, wakati naendelea na haja ndogo nikakumbuka andiko la mdau nikapepesa macho huku na kule nikaona camera imetegeshwa hata sikumaliza haja nikakatiza nikaipa camera mgongo nikanawa mikono na kwenda zangu, lakini pia camera nyingine imetegeshwa kwenye mlango.
Nilitamani kuwafuata wahusika kuwaambia kwamba kwa uamuzi waliochukua sio rafiki kwa faragha za watu lakini muda ulikuwa umeshaniacha maana nilikuwa nimechomoka kidogo kwenye majukumu kumleta mdogo wangu hapate huduma.
Naamini ndani ya jukwaa hili limekuwa likitusaidia kuwa huru kupaza sauti zetu na ninaimani hili suala tunatakiwa kulipigia kelele maana sio utaratibu tuliozoea maeneo mengi na naamini watu wengi wanaoenda kwenye vyoo hivyo bado hawajafanikiwa kuziona hizo camera, ni wachache watakaoziona wakawa huru kutumia vyoo hivyo.
Naomba wahusika kwenye hospitali hizo bila kujali sababu walizozingatia waondoe camera hizo, lakini watoke hadharani watueleze walikuwa na kusudi gani kisha watuombe radhi na kutuhakikishia kama faragha zetu zipo salama maana wanatufanya tuwaze mengi.
Pia soma
~ Naomba uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili uondoe CCTV Camera zilizowekwa chooni
~ Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi yaonya ufungaji wa Kamera (CCTV) kwenye maeneo ya faragha