Hospitali za REGENCY na TUMAINI zimulikwe!

Umesahau ile ya Usalama wa taifa kule PSU , halfu JK eti akapumzishwa hapo, huyu JK hajitaki?
 
Tumaini ndio sitaki kupasikia kabisa kuna shemeji yangu mmoja alijifunulia pale daktari hakuja kumuona mpaka mtoto akafariki it was so sad mama nae aliponea chupuchupu
 
Pole sana wote mlipata matatizo kutokana na huduma mbaya za hospitali zetu.

watanzania wenyewe inatupasa tuamke, tumezidi kulala, wananchi hatuna jitihada za kutaka mabadiliko, ndugu zetu wengi wanapoteza maisha kwa sababu ya uzembe, na kutanguliza pesa mbele, utu wetu umepote, hizi hosp zote zinazolalamikiwa zinapaswa kufungwa na uchunguzi kufanyika, waliopoteza ndugu zao waungane wawe kitu kimoja na kwenda wizara ya afya, media mbalimbali kutoa uozo ya hizo hosp

bado tunazidi kudanganywa kila wilaya, sijui kitongoji , sikjui kitu gani kutajengwa hosp, this is bull shit!, hizo zilizoko tu huduma ni mbovu, malalamiko ya wananchi kila kukicha.
 
Jamani hii habari imenisikitisha sana maana nakumbuka na mimi nimekuwa natibiwa sana pale Regency na kuna ndugu yangu alipoteza maisha akitibiwa pale ingawa sikusikia wakilalamika lakini nimejifunza kitu kikubwa sana kuhusiana na hizi hospitali zenye madaktari wa kuazima kutoka hospitali nyingine hasa Muhimbili.

NB: Poleni sana wafiwa mliopoteza ndugu zenu kwa uzembe huu, Mungu ndie mlipaji lakini kumbukeni kufanya mabadiliko katika uongozi ili kuleta matumaini mapya kwa Watanzania wengi wanaoteseka
 
Bora ya tumaini kuliko regency jamani regency kama wewe siyo muhindi au huna kitu hupati huduma,
 
Wakuu sasa kama mnajua mambo yako hovyo kiasi hicho kwanini hamchukui hatua za kisheria hasa kwa wanandugu waathirika.Kama kumbu kumbu zangu ziko sawa sawa Super Coach kalazwa Regancy,tafadhali wasilianeni na ndugu zake asije akapoteza maisha kabla ya siku zake.
 
Mwingine kafa leo alfajiri pale pale Regency, Naona hata nishai kwenda maana niliwaambia jamani ile si hospitali wakasema aaah wanawataalam toka India

Ntaenda kwenye mazishi tuu
 
namfahamu dada mmoja anaishi ughaibuni baba yake alikwenda agha khan mahututi ct scan ikaonyesha amepata CVA au stroke hiyo ilikuwa siku ya ijumaa wakamwambia aende nyumbani arudi juma tatu ,jumamosi asubuhi akafariki.Nimewashauri ndugu zake wafungue kesi ya wrongful death wanasema kesi haitaweza kumrudisha baba yao may be i am naive na mambo ya bongo its been a while but I don't understand it
 
Hakuwa mhindi nini maana Aghakan wahindi ndio kwanza wanaewa kipau mbele
 
Kweli kabisa,hata mimi nimepoteza ndugu yangu kwa uzembe wa hizi hospitali mbili.
 
Mkumbuke madaktari wa hizi hosp huwa ni wa part time toka muhimbili!hivyo huja regency au tumaini wakiwa wamechoka!
 
Siendi tena REGENCY coz hata mimi wameniboa sana juzi kati kwa huduma zao mbovu!!
 
Hospitali zinapogeuka kuwa magonjwa ya hatari! Zinahitajika specialization mpya za madaktari kuyakabili!
 
Tumwombe Mh. Kikwete aunde bodi ya AFYA kwa kweli, maana hata pale Hospital ya Morogoro mjina nakumbuka wakati tuko Chuo pale Moro, tulishawahi kumpoteza mwnezetu alikuwa anaumwa just tumbo, kufanya operation hakuamka. Ni vyema kukawa na sheria ya kulinda wat ambao hawana hatia....
 

ivi nyie watu, kuna mtu huwa anawafuata kuwachukua makwenu na kuwapeleka regency sijui tumaini au huwa mnaenda wenyewe??hospitals nyingi vimeo zimejaa mjini kwa sababu nyie mnaendelea kwenda huko na wao wanaendelea kuwaua..poleni kwa mliopoteza ndugu/wazazi/wapendwa wenu lakini all in all kama nyie wote hamtaenda huko hawa watu watakufa natural death kwa sababu they won't have customers sasa nyie mnazidi kwenda mnawapa kichwa na tena pamoja na kuwacharge mamilioni mnadhani hapo ndo mtapata good services?? au mnaitegemea serikali hii ya kisanii iseme tumaini na regency stop kwa sababu mnaviolate professional ethics?? mkiitegemea sserikali hii mtakufa wote, dawa ni kutotia mguu kabisa kunako hizi hospital, either watajiuliza na kujirekebisha au wataperish..u got to do something on ur own sometimes dudes!!
 

wee endelea kumtegemea kikwete ukija amka usingizini mtakuwa mshakufa wote..kikwete aunde bodi ana muda huo?? au unadhani yupo pale to serve pipo like u??wee endelea kuota mchana kweupe..
 
wajemeni kama mambo ni mabaya kiasi hiko nashauri serikali iweke kama rules hawa madaktari wawe wanaenda refresher courses kila mwaka,hii itatuhakikishia wako updated....wasiendelee kupoteza maisha ya watu hivi hivi.
 
Samahani sijakuelewa unaposema serikali inategemea mteremko kutoka hospitali za mission una maana gani? Kama unadhani hospitali zinazojiita za mission zinajiendesha fuatilia tena. Ni kutonye hospitali za misheni zinazoitwa cjui teule kama St Francis zinaendeshwa kwa 100% na Serikali.
 
Nilikuwa naenda Regency, lakini kwa stori hii, siendi tena!
 

Tanzania Heart Institute.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…