SoC04 Hospitali za Serikali na private ziwaajiri watu kwa ajili ya ushauri wa vyanzo vya magojwa

SoC04 Hospitali za Serikali na private ziwaajiri watu kwa ajili ya ushauri wa vyanzo vya magojwa

Tanzania Tuitakayo competition threads

rajabu musa

New Member
Joined
Apr 20, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Hii ina maanisha kuwa endapo serikali yetu kwa pamoja na mashirika binafsi au hospital binafs zinaajiri wataalamu kwa ajili ya kutoa elimu au ushauri kwa vyanzo vya magojwa hii itasaidia kupunguza mlundikano wa wagojwa katika hospital zetu.

Na hii ninachomaanisha hapo ni kwamba kila ugojwa unasababu zake hakuna ugojwa usio na chanzo chake mfano mzur juzi nmeenda hospital nikapima nikakutwa nina malaria ila cha ajabu ni kwamba nilipewa dawa tu kwa ajili ya kutibu malaria na kweli nmepona ila ninachokisema kuwa ni kweli tunapewa huduma nzuri ila hatushauriwi kuwa ili usiugue hii malaria tena inabidi ufanye yafatayo mfano wa kutumia neti kufyeka nyasi zilozpo karibu na nyumba unayokaa kufukia mashimo yenye kuweka majimaji ambapo ndipo mbu huzaliana n.k.

Mfano mwingine ni magojwa kama typhoid chanzo ni kula vitu vichafu maka matunda yasiyoosha na pia maji yasioyochemshwa n.k sasa unakuta kwel mtu ameenda Amepima na kapewa dawa na anapona vzur tu ila hospital pale hakuambia kuwa ili usiumwe tena huu ugojwa inakubidi uchemshe maji au pia kuepuka kula.vitu ambavyo havijaoshwa mfano matunda ili usiugue tena huwa vitu hivyo hatuambiwi na pia mtambua kuwa sio wote wanajua visababishi hivyo kwa hiyo ninachoshauriushi ni kwamba serikali yetu kama inaweza pia itoe ajiria kwa ajili ya wataalamu wa ushauri tu kwenye vituo vyetu hii itasaidia sana kupunguza au kutokomeza kabisa baadhi ya magojwa.

Pia serikali iweke utaratibu maalumu wa siku hata mara moja kwa mwezi wataalamu hao wawe wanapita nyumba hadi nyumba kutoa elimu kwa wananchi ili wananchi wawe na uwezo wa kujua na kutambua baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kuleta magojwa kwao.

Hii itasaidi pia kuepusha mlundikano wa wagojwa katika hospital zetu na pia hii itasaidi pia kukuza uchumi wetu kwa sababu endapo watu watakuwa wana elimu tosha kuhusu vyanzo mbalimbali vya magojwa inamaana pia watakiwa hawaumwi mara kwa mara na kama tunavyojua kuwa afya ndo mtaji hivyo badaya ya kwenda hospital watu watakuwa hawaumwi mara kwa mara na watakuwa wanafanya kazi zao na kuongeza pato la taifa kwa kulipa kodi.

Na pia serikali kwa kutumia wataalamu hao hao iweke mpango kuwa mgojwa anapofika kituo x na kugundulika kuwa ana shida flani lazima wataalamu wao wawe wanafanya mrejesho kwa kumfatitia huyo mgojwa na kuendelea kumpa elimu pia na sio tu mgojwa akifika hospital na kuwepo matibabu hakuna wataalamu wanaofalitia kujua je mgojwa alitumia dawa vizuri au pia hata kujua ushauri alipatiwa aliufanyia kazi au laa kwa kufanya hivyo tutapunguza wagojwa katika hospital zetu na badala yake watu watakuwa busy na kufanya kazi na sio kuugua.
 
Upvote 1
Sawa unashauri, waajiriwe watu.

Japo hata waliopo tambua kuwa wano wajibu wa kuwashauri watu kuhusiana na vyanzo vya tatizo. Vyuoni tunafundishwa vicious cycle of ill health na nini kifanyike.

Pamoja na kuwa ni wajibu, bado pia una haki ya kudai kuambiwa chanzo na taarifa zote kuhusu ugonjwa unaokusumbua.

Lakini je? Watanzania wapo tayari kupokea taarifa hizo. Nauliza kwa sababu wapo ambao huona kama unawapotezea muda na wapo wanaohisi unawadanganya rejea kauli anazopewa Profesa Janabi.
 
Back
Top Bottom