Hospitali za Umma ni kama lango la kifo

Hospitali za Umma ni kama lango la kifo

Andrew123

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2012
Posts
8,358
Reaction score
10,976
1. Ukifika hospital za Umma ni kama upo langoni kuelekea kifo.

2. Huduma mbovu, pengine mpaka utoe Chochote nimefika Mwananyamala mabango ya kukataza rushwa na makamera kila kona utadhani maonyesho Ila huduma hupati bila kutoa pesa ya chai au ujiandae kushinda hapo hospitalin toka asubuhi mpaka jioni.

3. Tubadilike. Zipo picha zaidi za ushahidi Ila hazifai kuweka hapa maana zinatweza utu.

4. Tuwatunze kw kuwapa huduma nzuri kinamama. Maana bila wao, tusingefika hapa.

NB: Land cruiser LC 300 sawa na 600m TZS unanunua vitanda vya chuma vingapi?
images (24).jpeg
 
Attachments

  • images (25).jpeg
    images (25).jpeg
    13.6 KB · Views: 6
Usiwalaumu saaana..... Ni urefu wa kamba tuu mkuu...

Wanachohubiri wanasiasa siyo uhalisia wa mambo kwa ground.

Ndiyo maana wakiumwa huwa hawaji hizo hospitali, wewe hujiulizi kwa nini?
 
Kama ile hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa jina maarufu General, nahisi ndiyo inaongoza kwa kushutumiwa kutoa huduma mbovu ndani ya Mkoa wa Dodoma.

Halafu ukija Wilaya ya Korogwe, kuna kitu kinaitwa Magunga hospital!! Hawa nao wajitathmini.

Yaani mpaka panadol nasikia wanakuambia ukanunue eti kwenye duka la dawa. Kila mzazi anayeenda kujifungua, analazimishwa kufanyiwa upasuaji!! Na wakati Wasambaa hawajazoea kabisa mambo ya aina hiyo.
 
Na hapo ni makao Makuu ya nchi
 
Watumishi wanaenda likizo bila kulipwa hela zao
Hawajapanda madaraja wengine
Mshahara mdogo na hakuna anayewajali
Sasa watafanyaje kazi kwasababu na wao ni binadamu.
 
Watumishi wanaenda likizo bila kulipwa hela zao
Hawajapanda madaraja wengine
Mshahara mdogo na hakuna anayewajali
Sasa watafanyaje kazi kwasababu na wao ni binadamu.
Taja majina yako matatu, tufuatilie madai yako
 
Nchi hii ina mambo ya ajabu sana, hasa muda wa kujifungua kama ni operesheni basi madaktari huwa wanajiona spesho sana, nilimpeleka wife Mnazi Mmoja wale madaktari wanadai rushwa wazi wazi!
 
Kwanini wasibinafsishe hizo hospitali za serikali.Maana hazina tija.Kama wafanyakazi Wana mgomo usio rasmi
 
Nataka Kiongozi ambaye atapunguza gharama za matumizi ya Serikali, atakubali kujinyima yeye na Serikali yake kusudi tu awapambanie Watanzania .

Ni nani huyo??.
 
Back
Top Bottom