Hospitali za Umma ni kama lango la kifo

Nilipata tatizo la appendicitis last last Friday nikiwa govt hospital wakati naanza taratibu za matibabu kuna Dr alienisomea majibu ya utra sound akaniambia kama unaweza nenda private hospital kwa procedures ndefu za humu ndani na hali Yako utakufa. Niliopt kwenda private na walini hudumia the same day na bahati mbaya walikuta ishapasuka,
 
Nataka Kiongozi ambaye atapunguza gharama za matumizi ya Serikali, atakubali kujinyima yeye na Serikali yake kusudi tu awapambanie Watanzania .



Ni nani huyo??.

Nipeni nafasi mimi niwe mtetezi wa wanyonge na Watanzania
 
Sitasahau mwananyamala mwaka 2007 mke wangu akiwa na uchungu wa kujifungua yupo ndani. Mimi nilikuwa nje na jamaa mmoja usiku sana ambaye hata hatukupeana namba lkn story zinaendelea.

HUko ndani kila mwanamke analia na lake kwa uchungu wa kujifungua, ghafla akatoka nesi akamwita jamaa yangu na kumpa taarifa kuwa mama na mtoto wamefariki.

Ilikuwa wakati mgumu sana kwangu lkn sikuwa na namna na hata asubuhi nesi ananitafuta nilikuwa na hofu sana kuwa ananiambia nini huyu dada.

Nashukuru Mungu wote wapo salama hadi hii leo lkn kila mtu alikuwa akiniuliza kwa nini nimeenda Mwananyamala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…