Hospitali zilinde Faragha za wagonjwa

Hospitali zilinde Faragha za wagonjwa

Kidagaa kimemwozea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
3,680
Reaction score
6,554
Nisahihi kwa hospitali kutoa Taarifa za wagonjwa wanaowafanyia matibabu kwa kubainisha Majina Yao, umri na mahali wanapoishi ?

Soma taarifa hii iliyochapishwa na EATV
#HABARI Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke imemfanyia upasuaji Zuwena Khamis Mwedadi mwenye umri wa miaka 51 mkazi wa Dar es salaam aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la uvimbe tumboni uliomtesa kwa miaka 16 tangu alipoanza kusumbuliwa na tatizo hilo mwaka 2008

Upasuaji huo umefanywa na jopo la madaktari watatu wakiongozwa na Dkt. Joseph Kiani akisaidiana na Dkt. Abdalallah Mashombo ambapo upasuaji huo umefanyika kwa muda wa saa (4) na kufanikisha kutoa Kilogramu 6.4 za uvimbe ukiambatana na kizazi

Akizungumzia upasuaji huo Daktari bingwa wa Magonjwa ya akina mama na uzazi Hospitali ya Temeke , Dkt. Joseph Kiani amesema mgonjwa huyo alipokelewa Hospitali ya Temeke na kufanyiwa vipimo mbalimbali ili kufahamu chanzo cha uvimbe huo ikiwemo kipimo cha CT Scan ndipo ilipogundulika ana uvimbe mkubwa lakini haikuonesha wapi uvimbe huo umeanzia kwasababu ulikuwa mkubwa sana

Dkt. Kiani anasema awali walishindwa kuendelea na upasuaji huo mapema kutokakana na mgonjwa kuwa na kiwango kidogo sana cha damu na hivyo kuendelea na kumpatia matibabu ya awali ikiwemo kumuongezea uniti tano za damu na ndipo wakaweza kumfanyia upasuaji

“Tulifanya vipimo kujiridhisha nini hasa chanzo cha uvimbe alionao, kwa muonekano wake uvimbe ulikuwa mkubwa kama mimba ya miezi tisa, baada ya vipimo tukafikia muafaka tumfanyie upasujai na hiyo ni baada ya kumuongezea damu kwa muda mrefu kwasababu alikuwa na kiwango kidogo cha damu cha g/dl 4 ambapo baada ya kufanya upasuaji ndipo tukafanikiwa kukuta uvimbe wenye kilogramu 6.4 na wote tumeutoa pamoja na kizazi” #EastAfricaTV
 
NI SAHIHI, Ila kwa ruhusa ya Mgonjwa au Ndugu wa mgonjwa.

Tofauti na hvyo hilo jambo sio sahihi.

Tanzania tunaishi kimazoea sana, ukiwa na akili timamu, muda na ukajua kutumia sheria vizuri. Kuna chance unaweza ukaishi kifahari kwa kulipwa fidia tu za kesi, kwa maana Nchi yetu vitu vingi haviendi kwa taratibu na kanuni zilizowekwa.

ULAYA kuna kampuni nyingi ambazo biashara yake ni kununua kesi, na hata hizi kesi unazoona nchi yetu inalipa mabillioni ya fedha, ni hizo kampuni zinakuwa zinanunua kesi kisha zinaweka mawakili wazuri na gharama za kesi wanasimamia then mwisho wa siku ukishinda kesi mnagawana fidia. so wao biashara yao miaka yote ni KESI.
 
Pt's Privacy and Confidentiality (Medical Ethics)

Kosa kubwa sana, akiwashitaki EATV na Madaktari hao tutaongeza Billionaire mwingine asubuuuhi kabisa wa kumfuatia Lissu.

#Akicheza na hii fulsa vizuri umaskini kwahell, Mungu anajibu Maombi.
 
Hospital gani wanamwaga ushuhuda kama kwa Mwamposa wanatafuta Fame eeh...?

Wangemwomba ruhusa kutumia kisa chake kama mfano bila kutaja utambulisho wake ingesound Ethical.
 
Nisahihi kwa hospitali kutoa Taarifa za wagonjwa wanaowafanyia matibabu kwa kubainisha Majina Yao, umri na mahali wanapoishi ?

Soma taarifa hii iliyochapishwa na EATV
#HABARI Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke imemfanyia upasuaji Zuwena Khamis Mwedadi mwenye umri wa miaka 51 mkazi wa Dar es salaam aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la uvimbe tumboni uliomtesa kwa miaka 16 tangu alipoanza kusumbuliwa na tatizo hilo mwaka 2008

Upasuaji huo umefanywa na jopo la madaktari watatu wakiongozwa na Dkt. Joseph Kiani akisaidiana na Dkt. Abdalallah Mashombo ambapo upasuaji huo umefanyika kwa muda wa saa (4) na kufanikisha kutoa Kilogramu 6.4 za uvimbe ukiambatana na kizazi

Akizungumzia upasuaji huo Daktari bingwa wa Magonjwa ya akina mama na uzazi Hospitali ya Temeke , Dkt. Joseph Kiani amesema mgonjwa huyo alipokelewa Hospitali ya Temeke na kufanyiwa vipimo mbalimbali ili kufahamu chanzo cha uvimbe huo ikiwemo kipimo cha CT Scan ndipo ilipogundulika ana uvimbe mkubwa lakini haikuonesha wapi uvimbe huo umeanzia kwasababu ulikuwa mkubwa sana

Dkt. Kiani anasema awali walishindwa kuendelea na upasuaji huo mapema kutokakana na mgonjwa kuwa na kiwango kidogo sana cha damu na hivyo kuendelea na kumpatia matibabu ya awali ikiwemo kumuongezea uniti tano za damu na ndipo wakaweza kumfanyia upasuaji

“Tulifanya vipimo kujiridhisha nini hasa chanzo cha uvimbe alionao, kwa muonekano wake uvimbe ulikuwa mkubwa kama mimba ya miezi tisa, baada ya vipimo tukafikia muafaka tumfanyie upasujai na hiyo ni baada ya kumuongezea damu kwa muda mrefu kwasababu alikuwa na kiwango kidogo cha damu cha g/dl 4 ambapo baada ya kufanya upasuaji ndipo tukafanikiwa kukuta uvimbe wenye kilogramu 6.4 na wote tumeutoa pamoja na kizazi” #EastAfricaTV
Mara nyingi huwa wanaomba kibali (informed consent) kwa mgonjwa tena kwa maandishi na anasaini. Kama hapendi taarifa binafsi ziwepo, yupo huru kukataa jina lake kuwepo
 
Sijaona cha ajabu au ambacho kinaathiri privacy ya mgonjwa hapo ,cha muhimu mgonjwa ameridhia taarifa zake zitoke Kwa umma Kwa maslahi ya taifa,hata ulaya Kila siku tunatangaziwa mgonjwa kapandikizwa moyo wa nguruwe,mara mwanaume kabadilishwa jinsia na wanatajwa hadharani lakini husikii watu waki react!juzi tu hapa tumesikia na kuona Baba wa Manara amefanyiwa oparesheni ya kuweka goti la bandia na ametangazwa watu hawajasema faragha yake imevunjwa?tuache ushabiki unless tuna ushahidi kama taarifa za mgonjwa zimetolewa bila idhini yake.
 
Sawa
 
Nisahihi kwa hospitali kutoa Taarifa za wagonjwa wanaowafanyia matibabu kwa kubainisha Majina Yao, umri na mahali wanapoishi ?

Soma taarifa hii iliyochapishwa na EATV
#HABARI Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke imemfanyia upasuaji Zuwena Khamis Mwedadi mwenye umri wa miaka 51 mkazi wa Dar es salaam aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la uvimbe tumboni uliomtesa kwa miaka 16 tangu alipoanza kusumbuliwa na tatizo hilo mwaka 2008

Upasuaji huo umefanywa na jopo la madaktari watatu wakiongozwa na Dkt. Joseph Kiani akisaidiana na Dkt. Abdalallah Mashombo ambapo upasuaji huo umefanyika kwa muda wa saa (4) na kufanikisha kutoa Kilogramu 6.4 za uvimbe ukiambatana na kizazi

Akizungumzia upasuaji huo Daktari bingwa wa Magonjwa ya akina mama na uzazi Hospitali ya Temeke , Dkt. Joseph Kiani amesema mgonjwa huyo alipokelewa Hospitali ya Temeke na kufanyiwa vipimo mbalimbali ili kufahamu chanzo cha uvimbe huo ikiwemo kipimo cha CT Scan ndipo ilipogundulika ana uvimbe mkubwa lakini haikuonesha wapi uvimbe huo umeanzia kwasababu ulikuwa mkubwa sana

Dkt. Kiani anasema awali walishindwa kuendelea na upasuaji huo mapema kutokakana na mgonjwa kuwa na kiwango kidogo sana cha damu na hivyo kuendelea na kumpatia matibabu ya awali ikiwemo kumuongezea uniti tano za damu na ndipo wakaweza kumfanyia upasuaji

“Tulifanya vipimo kujiridhisha nini hasa chanzo cha uvimbe alionao, kwa muonekano wake uvimbe ulikuwa mkubwa kama mimba ya miezi tisa, baada ya vipimo tukafikia muafaka tumfanyie upasujai na hiyo ni baada ya kumuongezea damu kwa muda mrefu kwasababu alikuwa na kiwango kidogo cha damu cha g/dl 4 ambapo baada ya kufanya upasuaji ndipo tukafanikiwa kukuta uvimbe wenye kilogramu 6.4 na wote tumeutoa pamoja na kizazi” #EastAfricaTV
Wacneni kukurupuka. Inawezekana jina la mgonjwa ni Fatuma ila madaktari wakatoa taarifa kwa kuficha na badala yake mgonjwa akapewa jina bandia Anna.
 
Back
Top Bottom