Hot story

wewe nini unajishaua kama hutaki watu wasome usingeiandika popote ungeiacha tu kichwani kwako hakuna ambaye angekuuliza
hiyo blog yako imezuia copy au ndio kujiona unajua sheria kumbe hujui lolote haya ifute hapa sio kulalama kama muimba taarabu

Hahahahaaa eti akiamua kumfungulia kesi..kesi gani ya kumshitaki mtu mwenye fake id?,hukumu itakua ban au?
Story katunga isomwe sasa analalamika nini?
 
mama facebook hana story moja hanazo nyingi sana so anamaanisha hizo nyingine itabidi ahandae kitabu ili guvu zake ziweze kumfaidisha kwani hapo kafanya vibaya.

Hapo namuunga mkono ,amalize hii halafu vitabu vingine tutanunua ila atutangazie tu kama kishatoka
 
Hapo namuunga mkono ,amalize hii halafu vitabu vingine tutanunua ila atutangazie tu kama kishatoka

Yaani mtu hadithi iko sehem.za mbele et unaikata utoe kitabu halaf hapo page zitaongezeka ngapi ilhali ushasoma mwanzo had ukapata uelewa akiamua kutoa kitabu asitoe hata mwanzo atangaze cover la kitabu na bei yake stor tutasoma wenyewe
 
wewe nini unajishaua kama hutaki watu wasome usingeiandika popote ungeiacha tu kichwani kwako hakuna ambaye angekuuliza
hiyo blog yako imezuia copy au ndio kujiona unajua sheria kumbe hujui lolote haya ifute hapa sio kulalama kama muimba taarabu

Halafu stor imeenea kote kama.vip asiwe anazotoa atoe makava ya vitabu mtu anunue akasome kwake alipoziachia huko.fb alijua watu wote wap fb kitu kimesambaa wosap kwenye mablog na huku jf hawez kuzuia watanunua watasoma na bado wataendeleza alipoacha
 
*****SORY MADAM*****(70)
AGE.............................................................18+
WRITER......................................................EDDAZARIA G.MSULWA

ILIOISHIA
"Alikuja nalo juzi usiku, ila kutokana sikuingia mchana zamu sijajua aliondoka vipi"
Nikajaribu kuuvuta mlango wa gari upande wa dereva na likafunguka.Nikaufunga mlango nikaondoka na kuwaacha walinzi wakiulizana maswali kadhaa, nikafika kwenye chumba cha kurekodia video zote zinazo chukuliwa na kamera za ulinzi.Sikuamini macho yangu baada ya kuwakuta wafanya kazi wawili wa chumba hichi, wakiwa uchi wa mnyama, wakifanya mapenzi na msichana, anaye onekana ni kahaba

ENDELEA
Walipo niona wakastuka, na kila mmoja akasimama sehemu yake, huku msichana wanaye fanya naye mapenzi akiziwahi nguo zake zilizo kuwa juu ya meza, na kujifunika katika sehemu zake za siri.Nikawatizama jinsi wanavyo babaika, sikutaka kuwasemesha kitu cha aina yoyoye zaidi ya kwenda zilipo computer nyingi
"Kuna video ninazihitaji"
"Sawa sawa bosi"
Akawasha computer moja, nikamuelezea, video ninayo ihitaji ni ile ya siku nilipokuwa ninafika hapa hotelini, nikaanza kuyaona matukio yote tangu nikiwa ninaingia na Phidaya sebleni, katika usiku ule nilimshuhudia John akizungumza na Victoria katika sehemu ya vinywaji, baada ya mimi na mke wangu kuingia ndani ya chumba chetu cha kupumzikia.Nikawaona wakiingia kwenye moja ya chumba ambacho si kile John alicho kichukua
"Mnamjua huyu?"
Nilimuonyesha John kwa kutumia kidole changu''
"Huyu ndio tunamjua, mara kwa mara huwa anakuja na mkurugenzi Victoria"
Nikaona mwanamke mwengine akiingia ndani ya chumba alichokuwa John na Victoria, huku akiwa amevaa baibui lililo mficha sura yake na kumbakisha macho tu
"Huyo aliye ingia ni nani?"
Jamaa akairudisha nyuma video, hadi sehemu anayo ingia mwanamke huyo ambaye, ndiye aliye mteka na kumuua mke wangu.
"Mlimuona kipindi akiingia ndani ya hicho chumba?"
"Hapana bosi"
"Iendeleze"
Jamaa akaiendeleza video, inayo onyesha watu wakiingia na kutoka kwenye vyumba vyao, kutokana na camera hizo zimetengwa kwenye kordo ya hoteli hii.Baada ya muda nikamuona John akitoka ndani ya chumba hicho, akaondoka zake, baada ya dakika chache akatoka Victoria na kuondoka, ila msichana huyo hakutoka hadi inatimu muda wa asubuhi ndipo naye akatoka, hapa ndipo nilipo ipata picha kamili kwamba kuna mchezo ambao ninachezewa na John pamoja na Victoria.Nikajikuta nikiwa ninahasira dhidi ya John na Victoria ambao wanaonekana wana siri kubwa sana waliyo ificha
"Huyo msichana alikwenda wapi?"
Wakanionyesha video ambayo tuliiangalia muda baada ya mke wangu kutekwa na msichana huyo ambaye hadi sasa hivi sura yake sikuweza kuijua
"Hembu nitolee hizo picha zake"
Jamaa akanitolea picha za msichana huyo aliye vaa baibui, kwa kutumia mashine ya ‘Printing' nikaikunja karatasi yenye picha ya msichana huyo na kuiweka mfukoni mwangu, nikatoka nje ya chumba na kurudi nilipo muacha dereva taksi, huku moyoni mwangu nikiwa ninahasira ya kwenda kutembeza kipigo kati ya John na Victoria hadi waseme ukweli ni wapi alipo mke wangu.
"Nirudishe kule tulipo anzia safari yetu"
Nilimuambia dereva taksi naye akatii, safari ikaanza kwa mwendo wa kawaida huku saa iliyopo kwenye simu ya John ikionyesha ni saa kumi na moja na dakika kumi, alfajiri.
"Ongeza mwendo dereva tuwahi kufika"
Nilimuamrisha dereva taksi, akazidisha mwendo kasi wa gari kutoka spidi ya themanini hadi mia moja na thelathini, gafla nikastukia kumuona derava taksi akipiga kichwa kwenye mskani wa gari, huku akitoa mlio wa maumivu, makali, gari ikayumba na kutoka kwenye barabara, huku vitu vigumu vikipiga kwenye kioo cha mbele cha gari, na upande wa pembeni wa gari.
Kwa akili ya haraka nikagundua kwamba ni risasi zinazo piga kwenye gari letu, lilili poteza muelekezo na kusababisha lizunguke kutokana na miguu ya dereva kufunga breki za gafla na kuyazuia matairi yote kutembea.Nikabaki nikiinama chini, huku nikijitahidi kuushika mskani wa gari kuhakikisha gari haizidi kupoteza muelekeo.Risasi zisizo ni milio ya bunduki zikazidi kumiminika kwenye vioo vya gari tulilopo, sikujua hata zinatokea wapi.Chakumshukuru Mungu, gari ikapiga kwenye mti mkubwa ulio pembezoni mwa barabara na kulisabaisha lisimame na kutulia.Mianga mikali ya taa za pikipiki nikaziona zikija kwa kasi kwenye sehemu gari lililopo
"Nimepona…….?"
Nilizungumza huku nikijipapasa mwili mzima, sikujihisi maumivu yoyote kwenye mwili wangu, zaidi ya vioo vingi, vidogo vidogo vilivyo vunjwa kwa risasi, kuniangukia kwenye koti nililo livaa pamoja na suruali yangu, kwa haraka nikajirusha kwenye siti ya nyuma ya gari, jamaa wenye pikipiki wakazidi kulisogelea gari nililomo.Sikutaka kujua kwamba dereva taksi ni mzima au amekufa, nilicho kifanya ni kuufungua mlango wa nyuma upande ambao gari imepiga kwenye mti.Nikatambaa haraka hadi nyuma ya mti na kujibanza, huku nikihema sana.Nikachungulia nikawashuhudia majamaa kama sita wenye pikipiki kubwa, wakiwa wamevalia makoti, makubwa meusi, huku wakiwa na bunduki mikononi mwao zilizo fungwa viwambo vya kuzuia sauti
Wakasimama mita chache kutoka lilipo gari, na kuanza kulishambulia tena kwa risasi, na kuzidi kunipa woga mwingi.Dakika kama tano hivi zikakata kwa majamaa kulishambulia gari letu kwa risasi, nyingi, nikachungulia kidogo, nikamuo jamaa mmoja akipiga hatua za taratibu hadi ilipo gari na kuichungulia ndani, na kuonekana akistuka sana
"Hayupo muhusika"
Alizungumza kwa sauti ya juu, huku akiwatazama wenzake, anaye onekena ni mkubwa wao akatoa simu, na kuminya minya na kuiweka sikioni, gafla simu ya Victoria ikaanza kutetemeka mfukoni mwangu, kutokana kuweka mlio ulio katika mfumo wa mtetemeko(vibration).Nikaitoa kwa haraka mfukoni mwangu na kwabahati nzuri ikawa imesha jipokea kotokana na kuibabatiza kwenye mfuko wangu wakati ninaitoa kwa haraka mfukoni mwangu, kutokana ni ‘screan touch' nikasikia sauti ikitoka kwenye simu iliyo pigwa ikizungumza kwa sauti ya juu kidogo
"Bosi muhusika hatujampata"
Maneno hayo yanafanana na jamaa anaye piga simu hiyo, nikachungulia na kumuona jamaa akiishusha simu yake kutoka sikiooni mwake
"Vipi"
"Bosi azungumzi chochote"
"Inakuwaje sasa?"
"Hivi mnauhakika hii ndio taksi, tuliyokuwa tukiifwatilia aliyo ipanda huyo Eddy?"
Mkubwa wao aliuliza
"Ndio hii, hembu mpigie bosi, kwenye ile namba yake nyingine"
Jamaa mmoja alimshauri mwenzake na kuinyanyua tena simu yake na kuiweka sikioni, nikajikuta nikiitumbulia mimacho simu ya Victoria nikisikilizia kuingia kwa simu hiyo.Ila haikuingia nikamsikia akizungumza
"Bosi tumemkosa Eddy"
"Tumefwatilia, tumefanya shambulio la gafla ila hatujamuona"
"Sawa, bosi"
Jamaa akakata simu na kuwatazama wezake
"Oya Jumbe, bosi anasemaje?"
"Anasema tuhakikishe tunarudi na kichwa cha Eddy, la sivyo atavikata vichwa vyetu"
"Mmmm"
Jamaa mmoja akaguna, huku akishusha pumzi nyingi, mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio, hapa ndipo nikapata uhakika wa Victoria ndio adui yangu namba moja na ndio yupo nyuma ya mpango mzima wa kumuua mke wangu akishirikiana na John, rafiki yangu wa karibu
"Kama atakuwepo atakuwepo eneo, haya tumt…….."
Kabla ya mkuu wao, anaye itwa Jumbe hajamalizia sentesi yake, sote tukastushwa na sauti ya simu ya John, iliyopo mfukoni mwangu.Nikasimama kwa haraka huku nikiwatazama jamaa, ambao nao wakanitazama huku akionekana kutokuamini macho yao, nisawasawa na mtu aliye okota embe dodo chini ya mti wa mpapai
"Kamaataaaaaaa mshenzi yule"
Jumbe alizungumza huku akininyoosheaa kidole, kwa haraka nikaanza kukimbia nikieleka kwenye msitu huu, ambao ulikuwa na barabara tuliyo kuwa tunapita.Taa za pikipiki wanazo ziendesha jamaa, zikazidi kunifwata kwa nyuma kwa mwendo wa kasi, nikazidi kukimbia kuelekea nisipo pajua huku nikikatisha katisha kwenye miti, nikikwepa risasi nyingi zinazo kuja nyuma yangu
"Eheee Mungu wangu, nisadie mie"
Nilizungumza huku nikiendelea kukimbia, nikafanikiwa kupandisha kwenye kilima chenye mawe mengi makubwa ambayo si rahisi kwa pikipiki kupita, nikazidi kuongeza mwendo wa kukimbia, huku nikihema sana, Nikazidi kupandisha mlima huku nikijitahidi kwa kadri yangu, kutafuta sehemu ambayo ninaweza kujibanza na kuwakwepa jamaa wana nitafuta
Nikafanikiwa kuingia kwenye moja ya mwamba wenye tobo kubwa, sikujali kama kunaweza kuwa na kutu cha hatari ndani ya mwamba huu, zaidi nilicho kijua mimi ni kujibanza huku, jasho jingi likinimwagika, kutokana na mwanga mzuri wa mbalamwezi nikawaona watu hao wakiendelea kutazama huku na huku na kuzidi kwenda mbele wakiamini kwamba nimekimbilia juu kabisa kwenye milima.Walipo potea kwenye macho yangu, nikaanza kurudi nyuma tulipo toka, safari hii nikijitahidi kufunga breki za miguu yangu, kuhakikisha sianguki kwani kasi niliyo nayo ya kushuka mlimani si ndogo, ikitokea bahati mbaya nikakosea kushuka nilazima kichwa kipige chini, hapo kuna mawili, kuvunjika vunjika mifupa au kufa kabisa
Simu ya John ikaanza kuita mfukoni mwangu, nikaitoa na kukuta jina la ‘My Victoria' huku pembeni kukiandikwa namba 2.Ikimaanisha ni namba ya pili kuwekwa kwenye simu hii, nikajibanza sehemu, yenye jiwe kubwa na kuitazama kwa muda, huku nikijaribu kuyalazimisha mate kupita kwenye koo langu lililo kauka kwa kiasi kikubwa, na taratibu nikaipokea na kuiweka sikioni
"Hahahaaaa, Eddy, rafiki yangu, si kila unaye muona kwako ni mwemaaaaa, wengine ni maadui.Kumbuka Tanzania wewe ulijifanya ni mjanja kunionea na kunidhalilisha kwa kunipiga, sasa ni muda wako wakudhalilikaaa, Ahahaaaaaaha"
Sauti ya John ilisikika huku, akizungumza kwa dharau na kucheka sana.Asira ikazidi kunipanda huku mwili mzima ukinitetemeka kwa hasira iliyo kali
"Ohhhh kaka Eddy, kumbuka mimi sio ndugu yako.Baba yako kwa nyege zake alimchukua mama yangu kutoka mikononi mwa baba yangu, kwa kutumia pesa zake, kisha wewe ukamtesa mama yangu na kumfanya afe, you're a loser…………"(….., wewe ni mpotezaji)
Sauti ya Victoria ilisikika huku wote wawili wakionekana kufurahia ushindi walio upata dhidi yangu
"Wait bro Eddy, ukirudi nyumbani utamkuta baba yako ni maiti, love you baby boy Eddy, mwaaaaaaa"(Subiri kaka Eddy……., nakupenda Eddy mtoto wa kiume,…&#8230😉
Nikajihisi, mwili ukipasuka kwa hasira nikataka kupiga hatua moja mbele, ila kuna kitu kigumu kikanigusa kwenye kichwa changu upande wa kulia
"Ohhhh lete simu yako"
Ni sauti nzito ya mmoja wa majambazi walio tumwa na Victoria, kuja kuniangamiza.Taratibu akapita mbele yangu, huku bunduki yake akiwa ameielekeza kichwani kwangu
"Utanaka simu eheeee"
Nilizungumza kwa kujiamini, huku nikimtazma kwa macho yaliyo anza kudondosha machozi ya asira pamoja na uchungu mwingi.Kwa haraka nikairusha simu juu, na kumfanya jambazi kuiangalia jinsi inavyo kwenda juu kwa kasi, nikaushika mkono wake wenye bastola, na kuvivunja vidole vyake vya mkono ulio shika bastola, akainama huku akitoa maumivu makali ya kuumia huku akilalamika.Nikampiga kigoti cha mso na kumfanya asimame, huku akiyumba yumba.Ngumi niliyo ikunja vizuri, ikatua kwenye shingo yake, ikampeleka chini, simu yake ya upepo aliyo kuwa ameishika na mkono mwengine ikaanguka chini huku sauti ya mkuu wake ikisisika
"G umepatwa na nini, eheeee"
Akanyanyuka na kutema mate pembeni yaliyo changanyikana na damu, ikiashiria kuna sehemu kwenye kinywa chake imepata itilafu.Akarusha teke, nikainama chini, na kujizungusha kwa haraka, nikaichota miguu yake na kumbwaga chini kama mzigo wa kuni.Macho yangu yakatua kwenye bastola iliyo anguka karibu yangu, nikaiokota kwa haraka, jamaa akanishika mguu wa kulia na kuuvuta, ikapelekea mimi kuangukia mgongo na kuichia bastola ikasogea pembeni kidogo.Jamaa akaniwahi kunikalia tumboni, akaanza kunikaba koo kwanguvu nyingi kwa kutumia mkono wake ambao sijauvunja vidole, nikajitahidi kuminyana naye, huku mkono wangu mmoja nikiupeleka ilipo bastola, Jamaa akazidi kuniminya koo langu, hadi nikajihisi kuanza kufanya mawasiliano na malaika mtoa roho
‘UKIWA MWANAUME HUTAKIWI KUKATA TAMAA KIRAHISI, PAMBANA HADI DAKIKA YA MWISHO, HATA KUUA IKIBIDI FANYA HIVYO, ILI TU UWE MSHINDI'
Nimaneno ya baba yangu mkubwa mzee Godwin, kipindi alipokuwa akinifundisha mazoezi ya kupigana, nilipokuwa kijana wa umri mdogo sana, na maneno yake haya alikuwa akiniambia pale anaponizidi ikiwemo kunipoga kabala.Nikazidi kuupelekea mkono wangu sehemu yanye bastola, kidole change kimoja cha katikati, mkono wa kulia, kikaanza kuivuta taratibu bastola, hadi ikafika kwenye vidole vyangu vyote vitano vya mkono wa kulia.Sikuuliza zaidi ya kuvuta traiga, ya bastola mara sita na kuziruhusu risasi sita kutoka kwenye bastola, na kupenya kwenye mbavu za jambazi huyu, akaanguka pembeni yangu huku akivuta pumzi yake ya mwisho
Nikasimama na kumtizama jambazi huyu jinsi anavyo hangaika hangaika, nikafyatua risasi mbili, zikaingia kichwani mwake, akatulia tuli, nikaiokota simu ya John pamoja na simu ya upepo ya jambazi iliyo anguka
"Upo wapi G wewe, tukufwate?"
Suti ya mkuu wao ambaye anaitwa Jumbe, ilisikika vizuri kwenye spika za simu hii
"Zamu yenu inafwata"
Nilizungumza kwa sauti nzito iliyo jaa mikwaruzo mingi, nikaipiga simu ya upepo kwenye jiwe kubwa, ikapelekea kuchanguka changuka vipande vingi.Nikakaanza kushuak kwenda chini, kwa bahati nzuri nikakuta sehemu walipo zisimamisha pikipiki zao, nikapanda kwenye moja ya pikipiki, nikaiendesha kwa kasi hadi umbali kidogo na zilipo nyingine, nikashuka na kurudi zilipo nyingine, nikaziangusha chini zote, nikazifungua mifuniko ya matanki ya mafuta, kisha nikarudi nilipo iacha pikipiki niliyo ichukua.Nikafyatua risasi mbili, zilipo pikipiki na kusabisha zilipuke zote
Nikaondoka kwa kasi, huku nikiotea otea njia ya kurudi barabarani, nikafanikiwa kutokeza kwenye barabara niliyo ifahamu, kwani ndio barabara kuu ya kurudi nyumbani kwa baba.Nikazidi konyeza mwendo kasi wa pikipiki, kimoyo moyo nikiapa kuwaua John na Victoria kwa mkono wangu mimi mwenye.Hadi ninafika nyumbani kwa baba imesha timu saa kumi na mbili asubuhi
"Nifungulieni geti nyinyi"
Niliwafokea walinzi wa getini, waliokuwa wakinihoji maswali, ikanilazimu kulivua kufia la pikipiki, ndipo wakanitambua ni mimi, wakafungau geti na kuingia ndani kwa kasi, walimzi wakabaki wakinishangaa, nikafika mlangoni na kuisimamisha pikipiki, kwa haraka nikashuka huku bastola yangu ikiwa mkononi, nikapandisha ngazi kwa haraka nikielekea kwenye chumba change, nikaupiga teke mlango, ukafunguka, chumbani sikukuta mtu zaidi ya kitanda kilicho changuliwa mashuka.Nikaelekea chumba cha Victoria, ila sikuwakuta.Nikaelekea chumba cha baba yangu, nikawakuta walinzi wake wawili wakiwa wamesimama mlangoni, ila mmoja akanizuia nisiingie
"Mzee amepumzika, hadi muda wake wa kuamka ukifika ndio, unaruhusiwa kuingia"
"Nini wewe"
"Hiyo ni sheria na si ombi"
"Unajua mimi ni nani?"
"Hata kama, ila muda wa mzee kuamka ni sambili kamili kwa sasa jaturuhusu mtu kuingia ndani ya chumba hichi"
Nikamshika tai mlinzi anaye nisemesha upuuzi wake, nikamvuta na kumuangusha chini, mwenzake akataka kunishika ila kwa haraka nikaielekeza bastola yangu, kwenye pua yake, akabaki kimya akinitumbulia mimacho yake.Nikausukuma mlango wa chumba cha baba, nikamkuta akiwa anazunguka zunguka kwenye feni lililo juu, huku akiwa amefungwa kwa kamba ngumu, mdomoni mwake akiwa amefungwa kwa plasta kubwa, huku miguu na mikono yake ikiwa imefungwa kwa kamba.Nikabaki nikiwa nimeduwa, nikastukia walinzi nilio gombana nao mlangoni wakinipita kwa kasi na kukimbilia anapo ning'inia baba na kuanza kumshusha huku wakiwasiliana na wezao kuomba msaada.Machozi ya uchungu yakaanza kunimwagika, walinzi wakazidi kujazana chumbani kwa baba yangu, huku daktari wake akijitahidi kumpatia baba huduma ya kwanza
Nikamuona daktari akitingisha kichwa baada ya kuweka sikio lake kwenye, kifua cha baba, na kukuta mapigo yake ya moyo yakiwa yamesimama, ikiashiria kwamba ni marehemu tayari.Sikutaka hata kukisogelea kitanda cha baba, nikatoka ndani ya chumba, huku nikiwa nimefura kwa hasira kali.Sikujua hata walipo John na Victori, na wao ndio wamesababisha mauji ya baba yangu.Simu ya John ikaita, na kukuta ni namba ngeni ndio inayo ita, nikaipokea haraka
"EDDDYYYYYYYYYY UPO WAPI KAKA"
Sauti ya John ilisikika kwenye simu
"Mshenzi, mpumbavu, nikikukamata nitakunyonga kama mulivyo fanya kwa baba yangu"
"Hhaahahaaaaa kumbe umefika nyumbani….Ohhhhh boy, huwezi fanya chochote kwani hujui nilipo"
"Kaka Eddy, mwaya samahani kwa kumuua baba yako"
Sauti ya Victoria ilisikika, alizungumza kwa dhara kubwa sana.Sikutaka kumjibu chochote, nikaikata simu, na kuingia kwenye mtandano wa goole, nika ‘download', apps inayoitwa google map pamoja na ‘mobile location tracker', inayo saidia kujua ni wapi namba ya simu iliyo pigwa inapatikana.Nikaiingiza namba ya simu iliyo nipigia, kitendo cha dakika moja nikafanikiwa kuletewa alama inayo onyesha ni wapi namba hiyo ya simu ipo na kuna umbali gani kutoka hadi sehemu nilipo.Nikatoka nje ya kupanda pikipiki yangu, na kuondoka kwa kasi, huku nikifwata jinsi simu inavyo nielekeza sehemu ninapoweza kuwapata John na Victoria
Ndani ya nusu saa nikawa nimefika kwenye moja ya mtaa, wenye watu wengi wanao onekana ni wavuta bangi, na sehemu niliyo simama pembeni kuna kundi la vijana walio choka choka na maisha, huku mmoja akiwa aimeishika simu ambayo alitumia John kunipigia, nikashuka kwenye pikipiki kwa kujiamini sana hadi sehemu walipo simama.Nikawasalimia ila hapakuwa na aliye ijibu salamu yangu, nikagusa bega aliye ishika simu akageuka, huku sura yake akiwa aimeikunja, akavuta fumba kubwa la msokoto wake wa bangi, kisha taratibu akaupulizia usoni mwangu, kitendo chake kikanipandisha hasira dhidi yake, nikampiga kidoti na sehemu za siri na kumfanya atoe ukelele, wezake wakataka kuingialia huku wakichomoa visu vyao, nikatoa bastola, nikawaelekezea moja baada ya mwengine akaanza kuondoka kwa kukimbia, akijaribu kuyaokoa maisha yake, nikabaki na mwenye simu
"Nani kakupatia hii simu?"
"Ehhheee?"
Nikamzaba kofi la shavu, hadi nikahisi na mimi maumivu makali kwenye kiganja change, kutokana nakutumia nguvu nyingi, jamba lililo sababisha vidole vyangu kujitokeza kwenye shavu la jamaa huyu
"Ni dada mmoja hiviii"
Jamaa alizungumza huku akilia, kama mtoto mdogo
"Huyo dada yupo wapi?"
"Sijui mimi"
Nikaikoki bastola yangu, na kuisokomeza mdomomi mwake, macho yangu yaliyo jaa asira yakazidi kumtazama jamaa huyu, ambaye mwanzoni alijihisi ni mbabe sana
"Na..ongea…."
Nikaichomoa bastola yangu mdomoni, ili kumpa nafasi ya kuzungumza
"Alimpa mtoto mmoja hivi, nikampokonya na kuichukua mimi"
Jamaa aliendelea kuzungumza huku akimwagikwa na machozi mengi
"Unanidanganya….?"
"Kweli, ila nawafahamu wale"
"Wanapatikana wapi?"
"Kuna godauni moja lipo hapo mbele, ndipo zilipo biashara zao"
"Twende unipeleke"
Nikaiacha pikipiki, tukaanza kutembea kwa miguu kuelekea lilipo godauni analo lizungumzia jamaa, hapakuwa mbali sana, tukafika kwenye moja ya jengo kubwa lenye geti kubwa
"Simama na ugonge"
Jamaa akasimama na kuaza kugonga, mimi nikasimam pembeni kodogo, huku nikiwa nimejificha.Geti likaanza kufunguliwa kwenda juu, akachungulia mlinzi mmoja mwenye bunduki mkononi mwake, sikutaka kuuliza zaidi ya kufyatua risasi iliyo tua kichwani mwa mlizi huyo, jamaa niliye kuja naye akaanguka chini kwa presha, nikaingia ndani ya godauni hili, lenye maboksi mengi, walinzi waliopo humu ndani wakanza kunishambulia kwa risasi, zilizo nikosa kutokana na kujificha kwenye nguzo moja,
"Stop fireee"
Niliisikia sauti ya Victoria ikiwaamrisha watu wake kuacha kupiga risasi, nikashusha pumzi nyingi huku nikilishuhudia geti likishushwa chini na kufungwa
"Eddy natambua kwamba ni wewe, hapo ulipo ninahesabu hadi tatu ninaomba ujitokeze"
Victoria alizungumza kwa sauti ya juu, niliyo isikia vizuri masikioni mwangu
"Mojaaaaaaa,"
Nikashusha pumzi nyingi, huku nikichungulia kuona sehemu alipo, sikuamini macho yangu baada ya kumuona John akiwa amemshika Phidaya, anaye lia, huku akiwa amemuwekea bastola ya kichwa
"Mbiliiiiiiiiiii"
Nikamtazama mke wangu aliye pauka sana uso wake, nikamtazama tumboni mwake na kukuta tumbo lake lipo vilevile, ikiashiria bado ni mjamzito
"Ta………."
Nikajitokeza kwenye nguzo niliyo jificha, walinzi kama hamsini, bunduki zao zote zikawa zimeelekea kwangu, nikaanza kutembea kuelekea katika sehemu walipo simama John, Phidaya na Victori, huku bastola yangu ikiwa mkononi mwangu
"Eddy mume wangu"
Phidaya akataka kunifwata, ila John akamshika nywele zake na kumvuta kwa nyuma, hadi akatoa ukelele akijaribu kuzishika nywele zake, John akaachia tabasamu pana usoni mwake, taratibu akianza kulishika tumbo la mke wangu.
"Eddy, umepata mke nzuri sana"
Victoria alizungumza kwa sauti ya dharau, John akamkumbatia Phidaya kwa nyuma, kitendo kilicho anza kunikasirisha, mikono ya John ikashuka taratibu hadi kwenye sehemu za siri za Phidaya, akaanza kumlazimisha kulifunua dera(gauni) lake, ili aizishike sehemu za siri za Phidaya, sikuvumilia kitendo cha John kumfanyia mke wangu unyama kama huo, nikaminya traiga ya bastola yangu, kwa bahati mbaya nikakuta bastola imeisha risasi, nikastukia nikipiga goti moja chini, huku damu zikianza kuvuja kwenye paja la mguu wangu wa kulia ulio pigwa risasi na John, aliye onekana kukasirishwa na kitendo change cha kujaribu kumuua
"Baby usimuue sasa hivi, bado hukumu yake"
Victoria alizungumza huku akimtazama John aliye fura kwa hasira nyingi, akitaka animalizie kunipiga risasi nyingine.Geti likafunguliwa, yakaingia magari manne aina ya BMW, zinazo fanana rangi, ambayo ni nyeusi yakasimama nyuma yangu, wakashuka wanaume nane walio valia suti nyeusi pamoja na miwani, maumivu ya mguu yakazidi kuniandama, huku kilio cha mke wangu, kikizidi kuniumiza.Akashuka mwanamke mmoja aliye valia suti yeusi, pamoja na kofia kubwa nyeusi, huku macho yake akiwa ameyafunika na miwani yeusi, nywele zake ndefu, zikiwa zimeufunika uso wake, akanipita na kusimama sehemu alipo simama Victoria, wakakumbatiana kwa furaha, kisha akaelekea sehemu alipo simama John, akamkumbatia huku wakizungumza chini chini.
Akageuka nyuma na kunitazama mimi, taratibu akavua miwani yake, akafwatia kofia lake kubwa, taratibu nywele zake akazisogeza pembeni, nikabaki nikistuka baada ya macho yangu kutazamana na macho ya Madam Mery.Mwalimu aliyekuwa mpenzi wangu kipindi ninasoma
"Mambo Eddy"
Alinisalimia huku akitabasamu, akpiga hatua za taratibu na kusimama mbele yangu, taratibu akachuchumaa, kidole chake kimoja akakiweka chini ya kidevu changu, kisha akazilete lipsi zangu karibu, akihitaji kunibusu, nikausogeza mdomo wangu pembeni, ila akanishika kwa nguvu na kuninyonya midomo yangu kwa kutumia nguvu, jambo lilizidi kumliza Phidaya mke wangu, madam Mery akaniachia na kusimama
"Mmmmmm ladha yako ya mate, imezidi kuwa tamu, baby wangu.Au huyu mwanamke wako wa kiarabu ameiongezea?"
Alizungumza kwa dharau, akamfwata Phidaya, nikastukia kumuona Phidaya akimzaba kofi la shavu Madam Mery, huku akisindikiza kofi hilo kwa mate yaliyo tua usoni mwa madama Mery, aliye anza kuchecheka kwa dharau.Madam Mery akampiga ngwala Phidaya, na kumfanya aangukie mgongo, na kutoa ukelele mkali wa maumivu, mguu mmoja wa madam Mery ukatua kifuani kwa Phidaya, madam Mery akanyoosha mkono, wake wa kulia akiomba kitu.Mlinzi wake mmoja akampa bastola, iliyo tengenezwa kwa dhahabu tupu.Akaikoki tayari kwa kumfyatulia mke wangu risasi
"MERY Tafadhali ninakuomba usimuue mke wangu"
Nilizungumza huku machozi yakinimwagika kwa uchungu mwingi, Phidaya akawa na kazi ya kulia huku akimuomba Mungu wake, amlaze mahali pema peponi
"Please SORRY MADAM, don't kill my wife…..Kama mtu wa kumuua ni mimi na si yeye"(Tafadali bibie, ninakuomba usimuue mke wangu……&#8230😉
Niliendelea kuzungumza huku machozi yakinimwagika kwa wingi usoni mwangu, Madam Mery akanitazama kwa macho makili kisha akmachia Phidaya, na kurudi nilipo simama mimi.
"Eddy, mimi ni mwanamke katili sana, ulikuwa hujui ni jinsi gani ninavyo mpenda Derick, ulimuua kinyama sana.Ulimkatakata kama kuku, na kumbanika.Wewe ni binadamu wa aina gani eheee? Unajua ni uchungu gani nilio upata juu ya kifo cha mume wangu wa ndoa Derick"
Madam Mery alizungumza kwa uchungu mwingi, huku aknitazama kwa macho makali sana, akanipiga teke la kifua, lililo niangusha chini, kwakutumia kitu chake chenye ncha kali ya kisigino, akanikanyaga kwenye jeraha langu na kuzidi kunipa maumivu pamoja na uchungu.Madam Mery akamngong'oneza Victoria, ambaye naye alimuuta mtu wake mmoja aliye ondoka katika eneo hili.
"Eddy nilikupenda ila siwezi kukuacha mzima hata kidogo"
Madam Mery aliendelea kuzungumza huku mara kadha akiniminya kwenye jeraha langu la risasi, meza kubwa ikaletwa na watu wa Vitoria, wakaninyanyua na kuniweka juu ya meza hiyo, wakanifunga kamba kwene kila mkono na ziichanua, huku watu wawili wakiwa wanazivuta kamba hizo, kila mmoja upande wake.Wengine wawili wakaifunga miguu yangu na kila mmoja akaivuta upande wake.
Jamaa mmojaa akamkabidhi madama Mery upanga wenye kumeremeta kwa rangi yake, madama Mery akapiga hatua hadi kwenye meza niliyo lazwa mimi, akanitazama kwa macho ya dharau
"Nafanya hii, kwa ajili yakulipiza kisasi cha mume wangu"
"Ngoja kwanza, nipo tayari kufa, ila ninakuomba usimuue mke wangu"
Nilizungumza kwa ujasiri, nikiwa nipo tayari kwa kufa, Madam Mery akalinyanyua panga lake juu, akalishusha kwa kasi kwenye mkono wangu wa kulia
ITAENDELEA KWENYE KITABU CHAKE KITAKACHO UZWA KWA SHILINGI 10000 TU
 

Mimi kama mimi sinunui
 

kuna mtu kamjaza upepo si bure...
 
Mhhhh!!! Humu JF story yoyote nzuri ikianza lazima zengwe litokee sijui kwanini??? Mpaka inaleta uvivu kusoma hizi story,.............yaani sijui kwanini??? Mnatutesa walevi sisi wa story.....wito kwa wote msiwe mnaleta story ambazo hamtakuja kuzimaliza,ukija na story uwe na uhakika wa kuimalizia,nisameheni bure kama nimewakwaza.
 

habari ndo hiyo sasa hapa wametusumbua tu
 
ujalazimishwa kununua mbona ni mtu wa shari sana wewe

Sikia nikwambie, hii hadith angeimaliza halafu angetangaza kitabu chake kingine, lazima watu wangenunua, lakin hii style Yake ya kataka kila mda abembelezwe hawez kufika
 
Mwambie kama anataka kuweka aweke kama hataki basi ila hatuwezi kununua kitabu hiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…